Manchester
United imeifunga Burnley 3-1 kwenye mchezo wa Premier League uliochezwa
Old Trafford na kukwea hadi nafasi ya tatu baada ya Southapton kubanwa
sare ya 0-0 na West Ham United kwenye mchezo mwingine wa Ligi Kuu.
Hata
hivyo mashabiki wa United bado wanaonekana kutoridhika na mfumo wa
kocha Louis van Gaal ambapo kwa muda kadhaa wakati matokeo yakiwa 2-1,
kundi fulani la mashabiki lilikuwa likizomea wachezaji wao.
Beki
Chris Smalling aliyeingia dakika ya tano kuchukua nafasi ya Phil Jones
aliyemia mwanzoni kabisa mwa mchezo, ndiye aliyefungia United mabao
mawili huku lingine likifungwa na Van Persie kwa njia ya penalti.
Phil Jones akificha uso kwa uchungu baada ya kuumia
Chris
Smalling anakuwa mchezaji wa kwanza kutokea benchi kufunga goli katika
kipindi cha kwanza katika historia ya Premier League.
Beki
huyo alifunga bao la kwanza dakika moja tu baada ya kuingia uwanjani
kabla Burnley hawajasawazisha dakika ya 12 kupitia kwa Danny Ings.
Smalling akatupia la pili dakika ya 45 wakati Van Perise alihitimisha ushindi kwa bao la dakika ya 82.
إرسال تعليق