Mbunge wa viti maalumu
kupitia chama cha demokrasia na maendeleo chadema CHIKU ABWAO akikagua jengo lilokumbwa na ajali ya moto
Mbunge CHIKU ABWAO akiwa katika eneo la nje ya jengo liloungua
Mbunge wa viti maalumu
kupitia chama cha demokrasia na maendeleo chadema CHIKU ABWAO alisikitiswa na
uongozi wa shule ya sekondari ya idodi
kushindwa kumpokea kama mbunge na mama aliyeguswa na ajali ya moto katika shule
kwa kuwa alikuwa ameshatoa taarifa kabla hajaenda katika shule hiyo.
Kitendo hicho kiliwafanya
baadhi ya wanahabari wa manispaa ya iringa waliokuwa wameongozana na mbunge
huyo walikasilishwa kitendo kilichofanywa na uongozi wa shule ya sekondari ya
idodi na walianza kuhoji je? angekuwa mkuu wa mkoa,mkuu wa wilaya na waziri au
mbunge wa jimbo hilo wangemfanyia hivyo.
Licha ya hujuma alizopewa
ambazo zinasadikika kuwa za kisiasa mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha
demokrasia na maendeleo chadema CHIKU ABWAO aliendelea na zoezi lake la kutoa
msaada wa shilingi milioni moja ili kusaidia majukumu mengine ya shule hiyo
kutokana tathimini fupi iliyotewa na baadhi ya walimu.
Akizungumza mbele ya
wanafunzi wa shule CHIKU ABWAO amesema
kuwa ameguswa na ajali hiyo ya moto ndio maana ameamua kujitolea kutoa msaada
huo.
aidha ABWAO ameishauri
serikali kujenga mabweni kwa mtindo nyumba za kawaida ili kuwawezesha wanafunzi kuishi kumi katika bweni moja
tofauti na sasa ambapo wanafunzi wanaishi zaidi ya mia na ishirini katika bweni
moja.
Lakini ABWAO akasisitiza kuweka ulinzi mzuri kwenye
mabweni kwa kuwa suala kama hilo limekuwa likijitokeza mara kwa mara katika
shule hiyo na kuomba wakandarasi watakao kuwa wanapewa tenda za kujenga mabweni
ya shule kuhakikisha wanaweka vifaa maalum vya kuzimia moto.
Alipotafuta mkuu wa shule kwa
njia ya simu na kuulizwa kwanini umemkimbia mbunge alijibu kwa kusema kuwa
alikuwa na majukumu mengine kwa hiyo sio lazima kumpokea mbunge wakati kuna
majukumu mengine makubwa zaidi ya yeye.
إرسال تعليق