Mchakato wa Katiba Mpya Wagubikwa na Rushwa

Mchakato wa kupata Katiba Mpya ya unadaiwa kugubikwa na wingu la ufisadi hali iliyosababisha Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) kuhoji tenda ya uchapwaji wa nakala milioni mbili za Katiba Inayopendekezwa kwa gharama ya Sh bilioni 6.
Hatua hiyo inakuja huku Watanzania wakiwa wanasubiri kupiga kura ya maoni inayotarajiwa kufanyika Aprili 30, mwaka huu, ambapo inaelezwa kuwa taratibu za manunuzi zilikiukwa kwa baadhi ya kampuni zilizopewa kazi hiyo.
Kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2011, taasisi zote za umma zinatakiwa zitangaze zabuni kabla ya kutoa zabuni husika.
Kutokana na sheria hiyo, inaelekeza taarifa za zabuni husika hutangazwa kupitia jarida na tovuti ya PPRA jambo ambalo linadaiwa halikufanywa na Wizara ya Katiba na Sheria.

Post a Comment

أحدث أقدم