Mtoto aliyenusurika kifo baada ya kukatwa kimeo

“Mwanangu aitwaye Leri (si jina halisi) mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi mitatu. Siku ya pili baada ya kumpeleka kwa mkata vimeo maeneo ya Kariakoo, nilikuwa na matumaini atapona kikohozi kumbe nimemuongezea matatizo. Hali yake ni mbaya.
Baada ya kukatwa, siku iliyofuata alikuwa akitema na kukohoa damu, nilipokuwa namtazama katika koo nikaona anatoa damu katika jeraha nikajipa moyo kuwa huenda damu hiyo itakata.
Lakini hali hiyo iliendelea, nikashtuka zaidi baada ya kuona mwanangu anapata choo chenye rangi nyeusi, ilipofika siku ya tatu akawa na homa kali, ndipo nikampeleke hospitali ya serikali (jina limehifadhiwa).
Mwanangu alitibiwa na kuongezewa damu mara mbili katika hospitali bado hali haikuridhisha.
Nilielezwa na madaktari kuwa jeraha alilopata baada ya kukatwa kimeo limeshindwa kugandisha damu na kuzuia damu isivuje.
Ikabidi apate rufaa kwenda Muhimbili ambako alipatiwa matibabu ya juu zaidi ili kutatua tatizo lake la damu kuendelea kuvuja.
Mama huyo anaeleza chanzo cha kumpeleka mwanaye kwa mganga wa kienyeji ni baada ya mtoto kuwa na kikohozi sugu.
Nilielezwa na shangazi zangu kuwa mtoto ana kimeo kirefu ndiyo maana anakohoa sana, hivyo akashauri akatwe kimeo na atakuwa na ahueni.
Alilalamika kuwa anajuta kumpeleka mwanae kwa watu wasio na utaalamu wa tiba kwa sababu badala ya kumtibu alimwongezea matatizo na kuhatarisha maisha yake.
Madaktari hospitalini
Wataalamu wa afya ya binadamu wanapata elimu iliyopitishwa duniani na kutumika miaka mingi katika kuelewa sayansi ya maumbile ya mwili, kazi zake na namna ya kutatua matatizo.
Wataalamu hawa huyasoma masomo ya tiba kwa muda mrefu na baadaye hupata usajili wa Serikali na kupewa leseni za kutibu.

Post a Comment

أحدث أقدم