Mtoto wa Beckham ana mambo!

STAA wa zamani wa England aliyewahi kutamba na Machester United kisha na Real Madrid, David Beckham amekiri kwamba mwanaye anayetabiriwa kufuata nyayo zake, Brooklyn, hana hamu na kampani yake.
Beckham ametoa siri hiyo katika kipindi kimoja cha televesheni alipokuwa akijibu swali juu ya nini familia yake imemwandalia Brooklyn katika sherehe ya siku ya kuzaliwa kwake itakayofayika mwezi ujao.
“Nadhani sasa anataka uhuru wa kuwa na marafiki zake, nadhani atakuwa na mlo wa jioni tofauti na ule wa familia. Kwa sasa yupo katika umri unaonyesha hahitaji sana niwe karibu naye, hapendi hata ninavyompeleka shuleni asubuhi, jambo siwezi kuliacha,” alisema.
Beckham (39), alisema bado anaamini kuwa ni wajibu wake kuwa karibu na Brooklyn ijapokuwa mwanaye huyo anaonyesha kutoendelea kufurahishwa na jambo hilo.
Kuhusu kutotakiwa kumpeleka shuleni, alisema: “Sijafurahishwa naye katika hilo kwa sababu nimekuwa nikiamka saa moja asubuhi ili kumpeleka darasani, ninapomwacha getini huwa namtakia masomo na siku njema.”

Post a Comment

Previous Post Next Post