SIKU chache baada ya mama wa mwanamuziki Diamond Platnumz,
Sanura Kassim kuripotiwa kuwa amelazwa nchini India kwa ajili ya
matibabu, meneja wa mwanamuziki huyo amesema hiyo itaendelea kuwa siri
ya familia.
Akizungumza na Mwanaspoti meneja huyo Hamis
Taletale maarufu Babu Tale alisema hiyo ni siri ya familia na hawawezi
kutoa majibu kuhusu lolote linaloendelea.
“Unataka kujua hali ya mgonjwa kwani wewe ndiye
unatoa dawa, hili ni suala la kifamilia na hatuwezi kulitangaza
magazetini,” alijibu babu Tale kwa kejeli.
Mama wa mwanamuziki huyo alipelekwa nchini India wiki mbili zilizopita kwa ajili ya matibabu baada ya kuugua ghafla
Post a Comment