MAHAKAMA
 ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo inatarajia kumsomea maelezo ya awali 
Mkurugenzi wa Sheria wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, 
Rugonzibwa Mujunangoma anayekabiliwa na kesi ya kupokea Sh milioni 323.4
 ambazo ni sehemu ya fedha zilizokuwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.
Mujunangoma
 anatarajiwa kupanda kizimbani na kusomewa maelezo ya awali mbele ya 
Hakimu Mkazi Emilius Mchauru kwa kuwa upelelezi wa kesi hiyo 
umekamilika.
Anakabiliwa
 na mashitaka ya kupokea Sh 323,400,000 kama tuzo baada ya kushughulikia
 masuala ya kampuni ya IPTL kama mfilisi, jambo ambalo linahusiana na 
kazi yake.
Katika
 mashitaka yake anadaiwa, Februari 5, 2014 katika jengo la Benki ya 
Mkombozi alipokea rushwa ya fedha hizo kupitia akaunti namba 
00120102602001 kutoka kwa mmiliki wa Kampuni ya Kufua Umeme ya VIP 
Engineering and Marketing ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya 
IPTL, James Rugemalira.
Inadaiwa
 fedha hizo ni sehemu ya zilizokuwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow. 
Mujunangoma yupo nje kwa dhamana baada ya kuwasilisha hati ya mali 
isiyohamishika yenye thamani ya nusu ya fedha anazodaiwa kupokea, pamoja
 na wadhamini wawili watumishi wa umma waliosaini hati ya Sh milioni 10 
kila mmoja.

Post a Comment