Mwanafunzi mmoja wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Idara ya sheria mwaka wa pili, Mathias Thimoth ametiwa mbaroni kwa tuhuma za wizi wa kompyuta mpakato ya mwanafunzi mwenzake.
Mathias Thimoth akiwa chini ya ulinzi.
Rais wa wanafunzi wa chuo kikuu hicho, aliyejitambulisha kwa jina
la Alfred Saluwa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo juzi alipozungumza
kwa simu na mwandishi wetu na akasema tayari suala hilo limeshafikishwa
polisi na uongozi wa chuo ameshauhabarisha.
...Akiingizwa kwenye gari.
Habari zaidi zinasema kwamba wanafunzi wengi chuoni hapo walikuwa
wakiibiwa kompyuta, hivyo wakaweka mtego ndipo mwananfunzi huyo
alipodakwa redi hendedi na mali hiyo. Hata hivyo, mara baada ya kukamatwa mwanafunzi huyo aliruka kimanga akidai kuwa yeye hahusiki na wizi wa kifaa hicho na akadai kwamba amebambikiziwa.
إرسال تعليق