Kijana mmoja, Omary Ramadhani, 28, (pichani) mkazi wa Sinza
Madukani, Dar amenusurika kifo baada ya kupata ajali ya kugongwa na
Break Down alipokuwa akiendesha Bajaj katika makutano ya Barabara ya
Sam Nujoma na Ali Hassan Mwinyi, Mwenge, jijini Dar es Salaam.
Kijana Omary Ramadhani anayedaiwa kuingizwa mochwari akidhaniwa amekufa.
Akizungumza kwa masikitiko, Omary alisema kuwa alipogongwa na gari
hilo hakuweza kujitambua kwani hata wasamaria wema walivyomchukua na
kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, walijua alifariki
dunia hivyo wakamuingiza moja kwa moja mochwari, lakini kwa bahati nzuri
alitokea nesi mmoja aliyeshauri asiwekwe kwanza kwenye friji mpaka
apimwe.
Akiendelea kuzungumza kwa tabu kutokana na maumivu ambayo anayo,
Omary alisema baada ya nesi huyo kumpima aligundua alikuwa akipumua kwa
shida.
Alisema hata ndugu zake walijua ameshafariki dunia kutokana na
alivyokuwa, kwani alivunjika mgongo mara sita na mfupa wa mkono ulitoka
nje na kupasuka kichwani jambo lililosababisha kuvuja damu nyingi.
Alifafanua kuwa kutokana na hali yake, alikimbizwa katika chumba cha
wagonjwa mahututi ambapo baada ya siku tatu alizinduka na walipokuja
ndugu zake aliwauliza alikuwa wapi, walipomuambia Muhimbili alizimia
tena.
Alisema alipata matibabu kwa muda wa miezi sita ndipo aliruhusiwa
kuondoka lakini alitakiwa atoe shilingi 1,000,000 kwa ajili ya tiba
maalum kwenye mashine ambayo siijui jina, lakini nimeshindwa kuzipata na
ndugu zangu ni walalahoi.
Omary alisema hivi sasa bado ana matatizo, haja ndogo haitoki sawasawa na akienda maliwatoni huchukua zaidi ya saa moja kwani mkojo hutoka kidogokidogo na kumsababishia maumivu makali ambapo haja kubwa anapata mara moja kwa wiki.
Omary alisema hivi sasa bado ana matatizo, haja ndogo haitoki sawasawa na akienda maliwatoni huchukua zaidi ya saa moja kwani mkojo hutoka kidogokidogo na kumsababishia maumivu makali ambapo haja kubwa anapata mara moja kwa wiki.
Omary amewaomba Watanzania wenye moyo wa huruma kumchangia ili
atibiwe, aepukane na mateso makali anayopata. Namba yake ni 0656 168
034.
إرسال تعليق