Baadhi ya wana CCM na Chadema kutoka kata ya Kilondo waliofika katika sherehe za miaka 38 ya CCM zilizofanyika kiwilaya kata ya Kilondo |
Boti iliyowabeba wana CCM na Chadema kwenda katika sherehe za miaka 38 ya CCM Ludewa ikiwa na rangi ya Chadema bendera ya CCM |
Mbunge Filikunjombe akiwa amebebwa juu juu kupelekwa meza kuu |
| |||
Vijana wa Chadema na CCM wakiwa wamembeba juu juu mbenge wa Ludewa Deo Filikunjombe alipowasili katika kijiji cha Kilondo kwa ajili ya sherehe za miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM kiwilaya kijijini hapo |
Vijana wa CCM na Chadema wakiwa wamembeba mbunge Deo Filikunjombe |
Mbunge Deo Filikunjombe akihotubia katika sherehe za miaka 38 ya CCM wilaya kwa wilaya ya Ludewa |
Mwenyekiti wa kijiji cha Nsele Bw |
Na matukiodaimaBlog
WANACHAMA wa
chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA ) na vyama mbali
mbali vya upinzani kata
ya Kilondo wilaya
ya Ludewa waungana
na wanachama wa chama
cha mapinduzi (CCM) wilayani hapo
mkoani Njombe
katika kusherehe miaka 38 ya
kuzaliwa kwa CCM
huku wakimchangishana kiasi cha
Tsh 100,000 mbunge wa
jimbo la Ludewa
Bw Deo Filikunjombe
kwa ajili ya kuchukua
fomu ya kugombea tena
ubunge mwaka huu katika
jimbo hilo .
Pamoja
na tukio la kuungana kwa pamoja
kusherekea miaka 38 ya kuzaliwa kwa
CCM na kumcghangia fedha
hizo mbunge wao bado
vijana wa vyama vya
CCM na Chadema walilazimika kumbeba juu juu umbali wa mita
500 mbunge Filikunjombe na mkuu
wa wilaya ya
Ludewa Juma Madaha huku
wakiwaita ni viongozi shujaa wa
wilaya ya Ludewa na Taifa la Tanzania
kutokana na kufika eneo
kijiji cha Nsele na kujitolea
kujenga Zahanati.
Tukio hilo la aina
yake katika Demokrasia na vyama
vingi nchini Tanzania
lilitokea juzi( Februari 15)
mwaka huu wakati wa wana
CCM katika wilaya ya Ludewa
walipofanya sherehe hizo kiwilaya
katika kata hiyo ya Kilondo kwa mara ya kwanza toka chama hicho
kilipoanzishwa .
Akisoma risala
ya wananchi
wa kata hiyo ya
Kilondo mzee Bernad Mwandesile (75)wa kijiji cha Nsele aliyeambatana wazee
wenzake 12 pamoja na diwani wa
kata ya Kilondo
Bw, Hilmary Mwakipokile.
walisema
kuwa wamelazimika kuwa wa kwanza
kumchangia kiasi hicho cha
fedha kutokana na kipimo cha uongozi ambacho wamempima ndani ya
jimbo hilo la Ludewa na jinsi anavyo watumikia vema
watanzania kwa ujumla
bungeni na kuwa ahsante yao kwa kazi kubwa anayoifanya ndani
ya jimbo hilo na
nje ya jimbo la Ludewa
wameona ni vema
wasimpoteze na badala yake
kumpa nafasi zaidi ya
kuwa mbunge wao.
“ Leo
hapa mbele yako
tupo wazee ambao tumewawakilisha vijana
na wannchi wote
wa kata yetu ya Kilondo kusema haya
na kukukabidhi rasmi
mchango wetu huu wa
Tsh 100,000 ili muda ukifika
ukachukue fomu tena ya kugombea
ubunge……tunajua kuwa kiasi
hiki cha fedha ni kidogo na hakitoshi kuchukulia
fomu ila uwezo wetu
umeishia hapo tunaamini kuwa
fedha nyingine nyingi utaongeza mwenyewe lakini leo pokea hiki kidogo toka kwetu “walisema wazee
hao katika risala yao kwa
mbunge Filikunjombe.
Kuwa
mbali ya mchango huo na imani
yao kubwa ya kutamani
jimbo hilo kuendelea
kuwa mikononi mwa mbunge huyo bado walikionya chama cha
CCM na viongozi wake
wa kitaifa kuwa
mbali ya mbunge huyo kutokea CCM ila wanamtambua kama
mbunge anayewafaa hata kama
angechukua fomu kwa Chadema ama chama
kingine chochote cha siasa au yeye
mwenyewe bila ya kusimama kwa chama chochote
bado wasingechagua mbunge
mwingine zaidi yake hivyo viongozi wa juu wa CCM wanapofanya maamuzi yao ya nani
asimame kugombea Ludewa pia wapime kwanza kuona
wananchi wanataka nini na nani
kwa ajili ya kuendeleza
wilaya ya Ludewa badala kuamua bila kujiuliza.
“……Tumepata kuwa na
wabunge hadi sasa toka
nchi hii ipate
uhuru mbunge Filikunjombe ni wa nane kuongoza jimbo la Ludewa
ila tuwe wakweli mbele ya
mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ludewa Stanley Kolimba ambae pia
nae yumo katika orodha ya
wabunge walioongoza jimbo la
Ludewa ….mbunge aliyefanya mambo makubwa kama haya ya
kimaendeleo zaidi ya Filikunjombe
hayupo …kweli tumempata anayecheka
na sisi
wakati wa furaha na kulia na sisi
wana Ludewa wakati wa shida hatuna haja ya
hao wanaojipitisha kwa kutaka kutuvuruga mlango tunaufunga kwa
kumwomba Deo Filikunjombe
kuchukua fomu tena pia mbali ya
jina lako maarufu la jembe
letu wana Ludewa
bado tunaomba kukubatiza upya hapa
leo kuwa utaitwa “Msamaria mwema” kuanzia leo hii ni
kutokana na moyo wako
wa utoaji ”
Wazee
hao waliowakilisha wenzao ni pamoja
Joseph Mwembeleko, Annastasia Lupangaro, Abel Mwakipokile,
Stanlaus Mwambeleko, ,Melenia Kilongo, Emmanuel Mwakipokile, Yordan Mwafingulo,,Sailis Ipungu,Maria Ngailo
,Bernad Mwansesile na diwani wa
kata hiyo Hilmary Mwakipokile.
Awali diwani
wa kata hiyo ya Kilondo Bw ,Hilmary Mwakipokile pamoja
na kuomba radhi
kwa mbunge Filikunjombe mbele
ya wananchi wake kwa kutoshiriki katika sherehe
kubwa ya uzinduzi
wa mradi wa umeme REA
kata ya Kilondo uliozinduliwa katika kijiji cha Kilondo wiki moja
iliyopita kwa madai ya kuwepo
kikazi nje ya wilaya ya
Ludewa bado alisema wapo
baadhi ya wana CCM wamekuwa wakipeleka taarifa zisizo sahihi kwa mbunge
huyo kwa lengo la kumchafua
kwa kudai hayupo pamoja na
mbunge jambo ambalo si
kweli na yeye hawezi kuwa mwanachama mwingine yeyote anayetaka ubunge
zaidi ya Filikunjombe .
“Nataka kukuhakikishia mbunge nimepita vijiji
vyangu vyote na kuitisha mikutano na kukutana na
wazee na kuomba radhi kwa kutokuwepo siku ya uzinduzi wa
mradi wa umeme kweli nipo nyuma yako
na kuendelea kuunga
mkono kwa nguvu zote shughuli za
kimaendeleo unazoendelea kuzifanya hapa
kata ya Kilondo ulipounga
mkono ujenzi wa Zahanati ya Kilondo
mimi pia nimekuunga mkono
kwa kuchangia mifuko 8 ya
saruji “
Mwenyekiti wa CCM
wilaya ya Ludewa Stanlye Kolimba mbali ya
kumpongeza mbunge Filikunjombe
kwa kazi nzuri ya kukijenga
chama katika wilaya ya
Ludewa bado aliwatoa
hofu wananchi wa
Ludewa kuwa lengo la CCM ni kuwatumikia
wananchi kwa kuwasogezea miradi
ya kimaendeleo hivyo CCM hakitapuuza matakwa ya
wananchi juu ya mbunge wao huyo.
Akiwashukuru kwa
mchango huo wa fedha ya kuchukulia
fomu mbunge Filikunjombe alisema
kuwa amefarijika zaidi kwa moyo
wa upendo walionyesha
wananchi hao wa kata ya
kilondo na kwa kuwa
wamemtangulia kumwomba
kugombea ubunge kabla ya muda kufika na
yeye kutangaza popote kama atagombea tena ama
hatagombea ubunge kwa mara ya
kwanza anawatangazia kuwa bado
anaupenda ubunge hivyo muda
ukifika atachukua tena fomu.
“Sijapata
kutamka sehemu yoyote kama
nitagombea tena ubunge ila leo wananchi
wa kata ya Kilondo mmenipa
moyo sana maana pale
vijana waliponibeba juu juu walianza kuvutana wenyewe kwa wenyewe
kwa wale wa Chadema
kuniomba kuwa mheshimiwa tunakupenda
sana tunaomba CCM wakikukata
jina lako ugombee kwa chama
chetu …… huku wale wa CCM
wakisema hakatwi mtu wewe wetu ila uamuzi huu wa
wazee kuamua kujichangisha na kunipa
fedha ya
kuchukua fomu ….kweli sitapata
kutangaza popote na muda bado wa kufanya hivyo ila nasema kwa moyo na upendo huu mlionipa leo nasema
nitagombea tena ubunge “
Mbunge Filikunjombe
alisema mbali ya kuwa
sherehe hizo ni za CCM ila ameshangazwa sana na kuvutiwa na
wananchi wote wa kata hiyo kuacha
shughuli zao na kufika kumpokea
na kusherekea miaka 38 ya CCM jambo ambalo ni kielelezo tosha kuwa wanampenda .
Alisema katika
kusogeza maendeleo kata hiyo
ya Kilondo amelazimika kujitolea kujenga
zahanati ya kijiji
cha Nsele pamoja na kukabidhi
vifaa mbali mbali kama magodoro
25 kwa Zahanati ya Kilondo ambayo wagonjwa
walikuwa wakilala chini ,
Sementi, mifuko 150,bati za kutosha zahanati
inayojengwa na kulipia mafundi wanaojenga
zahanati hiyo na kufanya
jumla ya thamani ya msaada
wote kufikia zaidi ya Tsh milioni 13.
Kwa upande
wake mkuu wa wilaya ya Ludewa Juma Madaha pamoja na kumpongeza
mbunge huyo kwa kuwasaidia
wananchi hao ujenzi wa
Zahanati pia aliahidi
kumuunga mkono kwa kuchangia
kiasi cha Tsh 500,000.
MWISHO
إرسال تعليق