Jeshi
la polisi mkoani Tabora limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa matukio ya
uhalifu katika kata ya Ngambo manispaa ya Tabora, akiwa na risasi 356 za
silaha za SMG/SAR.
Jeshi
la polisi mkoani Tabora limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa matukio ya
uhalifu katika kata ya Ngambo manispaa ya Tabora, akiwa na risasi 356 za
silaha za SMG/SAR, zinazosadikiwa kuwa, zilikuwa zitumike, katika
matukio ya uharifu katika mikoa ya Tabora, Kigoma, Mbeya, na Njombe.
Kaimu kamanda wa polisi mkoani Tabora ACP Juma Bwire amemtaja
mtuhumiwa huyo kwa jina la Warfram Benard Msemwa, mkazi wa Sikonge,
ambaye alikuwa akitafutwa na jeshi hilo kutokana na kutelekeza begi
lililokuwa na silaha aina ya SMG na risasi 17, katika eneo la kituo cha
afya cha mazinge wilayani humo.
Aidha ACP Juma Bwier amesema kuwa, katika kumhoji mtuhumiwa huyo
amekiri kuwa na mawasiliano ya kiuharifu na watu fulani katika nchi
jirani ya Burundi ambapo zinatoka risasi hizo pamoja na silaha, ambayo
aliitelekeza hapo awali kwa kuwahofia polisi aliowaona kwa mbali.
Amesema kuwa upelelezi ukikamilika mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani.
Post a Comment