Polisi Tabora yamkamata mtuhumiwa sugu wa ujambazi

Jeshi la polisi mkoani Tabora limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa matukio ya uhalifu katika kata ya Ngambo manispaa ya Tabora, akiwa na risasi 356 za silaha za SMG/SAR.
Jeshi la polisi mkoani Tabora limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa matukio ya uhalifu katika kata ya Ngambo manispaa ya Tabora, akiwa na risasi 356 za silaha za SMG/SAR, zinazosadikiwa kuwa, zilikuwa zitumike, katika matukio ya  uharifu katika mikoa ya Tabora, Kigoma, Mbeya, na Njombe.
Kaimu kamanda wa polisi mkoani Tabora ACP Juma Bwire amemtaja mtuhumiwa huyo kwa jina la Warfram Benard Msemwa, mkazi wa Sikonge, ambaye alikuwa akitafutwa na jeshi hilo kutokana na kutelekeza begi lililokuwa na silaha aina ya SMG na risasi 17, katika eneo la kituo cha afya cha mazinge wilayani humo.
Aidha ACP Juma Bwier amesema kuwa, katika kumhoji mtuhumiwa huyo amekiri kuwa na mawasiliano ya kiuharifu na watu fulani katika nchi jirani ya Burundi ambapo zinatoka risasi hizo pamoja na silaha, ambayo aliitelekeza hapo awali kwa kuwahofia polisi aliowaona kwa mbali.
Amesema kuwa upelelezi ukikamilika mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani.

Post a Comment

أحدث أقدم