Pichani
Malaria akiwa amejipumzisha kwenye kibaraza cha maeneo ya ofisi za
Idara ya Habari Maelezo kama alivyokutwa na mpiga picha wetu.
Na Andrew Chale, modewjiblog
Hali
ya sintofahamu juu ya mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la ‘Malaria’,
imezidi kuwa kero kwa baadhi ya watu ikiwemo wanawake kwa mtu huyo
kuwafanyia vitendo vya kidhalilishaji kwa kuwashika sehemu nyeti, na
baada ya hapo kukimbia ama humtisha kwa lengo la kutaka kumpiga
aliyemfanyia kitendo hicho.
Kwa siku kadhaa, modewjiblog imekuwa
ikifuatilia mienendo ya mtu huyo ambaye pia inasemekana kuna wakati
huwa anarukwa na akili hali iliyopelekea kuitwa jina hilo la Malaria.
Baadhi ya watu walioongea na modewjiblog
walieleza kuwa, Malaria amekuwa kero kubwa kwa wanawake na wasichana
hasa wanaopita usawa wa ukumbi wa Idara habari MAELEZO na maeneo jirani
ambapo huwanyatia na kisha kuwafanyia vitendo vya kidhalilishaji na
kisha kukimbia.
Salum
Ally ambaye ni Dereva Taxi, eneo hilo la MAELEZO, alibainisha kuwa, mtu
huyo amekuwa akipigwa mara kwa mara na hata kupelekwa Polisi, lakini
baada ya siku kadhaa anarejea maeneo hayo.
“Huyu
mtu amekuwa kero sana hasa kwa vitendo vyake vya kuwashika makalio
wanawake pamoja na maziwa. Imekuwa hofu kubwa sana lakini mamlaka husika
wanashindwa kuchukua hatua za haraka” alibainisha Salum.
Malaria
akiomba msaada wa hela kwa mmoja wa wanawake waliokua wamesimama karibu
na maeneo ya ofisi za Habari Maelezo katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Kwa
upande wake, Monica Dorcas ambaye anafanya shughuli zake za kuuza vocha
alibainisha kuwa, kwa sasa Malaria ameibua hofu kubwa kwani, wakati
mwingine humvizia mwanamke hata kama amemuona mbali na kisha kumfanyia
vitendo hivyo.
“Kwa
sasa akiona pia mwanamke amevaa nguo za kubana ama ana maumbile
makubwa kama amemuona toka mbali ama amempitia karibu yake, humfuata
nyuma nyuma na kisha humshika makalio na kukimbia” alisema Monica.
pia tulishuhudia vitendo hivyo vya kudhalilisha wanawake hao, ambapo endapo
ataona anashindwa kutimiza adhma yake hiyo, Malaria hujifanya
anamsalimia ama kumuomba msaada wa pesa ama kumuongelesha na kisha
mwanamke ama msichana akijisahau humshika maziwa ama makalio na
kukimbia.
Aidha,
imebainika kuwa, mbali na kufanya vitendo hivyo, pia Malaria anatembea
na sindano ama pini zenye ncha kali, ambapo huvizia wanawake na
kuwachoma. Ambapo inadaiwa kuwa mwaka jana aliwahi kutenda tukio la
kumchoma mwanadada mmoja sindano, hali iliyopelekea kupigwa na kuwekwa
ndani, lakini baadae walishangaa amerejea tena, ambapo yupo
akirandaranda katikati ya jiji hasa maeneo hayo ya MAELEZO.
Tunatoa wito kwa mamlaka husika kuchukua hatua za haraka juu ya mtu
huyu, kabla ya matatizo zaidi hayajatokea kwa sasa kwani amezidi kuwa
kero kwa watu wote.
إرسال تعليق