Tamsha la Sauti za Busara kusheheni Wasanii Nyota wa Nje na Zanzibar kurindima Ijumaa viwanja vya Ngome Kongwe Zenj

Afisa Habari wa Sauti ya Busara Zanzibar Ndg.Dave Ojay Haashim, akitowa maelezo ya matayarisho ya Tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika Ijumaa hii katika viwanja vya Ngome Kongwe Zanzibar wakati wa Mkutano na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar katika ukumbi wa hoteli ya Grand Palace Malindi Unguja leo.
Msanii Rico Single na Msanii Mkongwe Zanzibar Bi Maryam Hamdan, wakiwa katika ukumbi wa mkutano huo wakifuatilia 
Mwenyekiti wa Sauti ya Busara Zanzibar Mhe, Simai Mohammed Said, akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kukamilika kwa matayarishi ya Tamasha la Kimataifa la Sauti za Busara Zanzibar, linalitarajiwa kufanyika wiki hii katika viwanja vya Ngome Kongwe Zanzibar na kuwashirikisha Wasanii maarufu kutoka Nje ya Zanzibar na Wazanzibar akiwemo Msanii wa Kizazi kipya ZenjFlava Rico Single.
Mkurugenzi wa Busara Ndg. Yussuf Mahmoud, akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali Wasanii watakaoshiriki Tamasha hilo,na Vikundi vya Kimataifa vya ngoma za Utamaduni kutoka nje ya nchi na ndani, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Grand Palace malindi Zanzibar. 






 


Post a Comment

أحدث أقدم