Afisa Habari wa Sauti ya Busara Zanzibar Ndg.Dave Ojay Haashim, akitowa
maelezo ya matayarisho ya Tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika Ijumaa
hii katika viwanja vya Ngome Kongwe Zanzibar wakati wa Mkutano na
waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar katika ukumbi
wa hoteli ya Grand Palace Malindi Unguja leo.
Msanii Rico Single na Msanii Mkongwe Zanzibar Bi Maryam Hamdan, wakiwa katika ukumbi wa mkutano huo wakifuatilia
Mwenyekiti wa Sauti ya Busara Zanzibar Mhe, Simai Mohammed Said,
akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kukamilika kwa
matayarishi ya Tamasha la Kimataifa la Sauti za Busara Zanzibar,
linalitarajiwa kufanyika wiki hii katika viwanja vya Ngome Kongwe
Zanzibar na kuwashirikisha Wasanii maarufu kutoka Nje ya Zanzibar na
Wazanzibar akiwemo Msanii wa Kizazi kipya ZenjFlava Rico Single.
Mkurugenzi wa Busara Ndg. Yussuf Mahmoud, akizungumza na waandishi wa
habari wa vyombo mbalimbali Wasanii watakaoshiriki Tamasha hilo,na
Vikundi vya Kimataifa vya ngoma za Utamaduni kutoka nje ya nchi na
ndani, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Grand Palace
malindi Zanzibar.
Post a Comment