VIONGOZI
wa madhehebu mbalimbali ya dini nchini wametakiwa kuacha tabia ya
kuwakumbatia na kuwanadi baadhi ya wagombea wa nafasi mbalimbali za
uongozi mbele ya waumini wao kwa kutumia nyumba za ibada.
Rai
hiyo ilitolewa jana mjini Songea na Mwenyekiti mpya wa Serikali ya Mtaa
wa Making’inda, Hashim Asham alipokuwa akizungumza na wanawake wa mtaa
huo wakati wa uzinduzi wa Chama cha Akiba na Mikopo (Saccos) ambapo pia
amewasihi viongozi hao kuahamasisha waumini wao kujitokeza kuipigia kura
Katiba Iliyopendekezwa.
Alisema
baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa na tabia ya kuwafanyia kampeni
wagombea wanaowataka wao, jambo linaloweza kuibua mitafaruku mikubwa
katika nyumba za ibada.
Alisema
viongozi hao wamekuwa wakijihusisha na siasa huku wakitumia nyumba za
ibada na kushabikia waumini kuchagua aina fulani ya wagombea, jambo
alilosisitiza ni kinyume cha maadili ya kazi zao.
Katika
uzinduzi huo uliohudhuriwa pia na viongozi wa dini, alisema viongozi wa
aina hiyo hawajui wanachokifanya, kwani wanaacha majukumu yao ya msingi
badala yake wanaingilia kazi za watu wengine na yanaweza kuwagharimu
kwani kuzomewa au matusi ni jambo la kawaida kwa wanasiasa, lakini sio
kwa viongozi wa dini.
إرسال تعليق