Umoja wa wafanyabiashara ndogo ndogo Ubungo jijini
Dar es Salaam, wameujia juu uongozi wa Manispaa ya Kinondoni kutokana na
vitendo vya kufukuzwa na kunyang’anywa bidhaa zao kabla ya manispaa
hiyo haijawatafutia maeneo mengine ya kudumu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana,
Mwenyekiti wa umoja huo, Honoratha Mashoto, alisema Manispaa ya
Kinondoni iliahidi kuwapatia eneo la Simu 2000 kwa ajili ya kufanyia
biashara zao.
“Hatupendi kuhangaika barabarani na kupambana na mgambo wa Manispaa
mara kwa mara kama raia huru wa nchi hii na wala si wakimbizi kwenye
nchi yetu. Tunaomba tuwe na kituo rasmi na cha kudumu cha kuendeshea
biashara zetu kwa amani na utulivu na siyo kukimbizana kila siku,”
alisema.
Alisema wanamuomba waziri mwenye dhamana aishinikize Manispaa ya
Kinondoni kutumia eneo la ekari nne zilizobaki kwenye kiwanja Na.
2005/2/2. Kitalu ‘C’ Sinza eneo la Simu 2000 kinachomilikiwa na
Halmashauri ya Manispaa kwa ajili ya wafanyanyabiashara ndogo ndogo.
Hata hivyo, Msemaji wa Manispaa ya Kinondoni, Sebastian Mhowera,
alisema hautambui umoja huo kutokana na kufanya biashara sehemu zisizo
rasmi

إرسال تعليق