Washitakiwa
wa kesi ya mauaji ya mjumbe wa Tume ya Taifa ya Mabadiliko ya Katiba,
Dk Sengondo Mvungi wameiomba Mahakama iwape haki ya kuwasikiliza.
Wanadaiwa
kuwa Novemba 3, mwaka juzi katika eneo la Msakuzi, Kibwegere wilayani
Kinondoni jijini Dar es Salaam, walimuua Dk Mvungi kwa kukusudia.
Waliwasilisha
ombi hilo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu
Mkazi Waliarwande Lema wakati kesi hiyo ilipotajwa na Wakili wa
Serikali, Leonard Challo kudai upelelezi bado haujakamilika.
Mshitakiwa
Longishu Losingo alidai wapo jela, lakini wanatakiwa kupata haki zao za
msingi kwa sababu wanaona Mahakama inaegemea upande mmoja, hoja zao
hazisikilizwi.
Hakimu Lema alisema hawezi kuwasikiliza na alishatoa kibali waende kwa Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo.
Aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 23, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.
Aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 23, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.
Mbali
na Longisho, washitakiwa wengine ni Chibago Magozi (32), John Mayunga
(56), Juma Kangungu (29), Paulo Mdonondo (30), Mianda Mlewa (40) ,
Zacharia Msese (33) Msigwa Matonya (30) na Ahmad Kitabu (30).
إرسال تعليق