Muonekano wa mbele wa gari hilo lililopata ajali.
Muonekano wa chini ya gari baada ya kupinduka.
Matofali yaliyokuwa kwenye gari hilo yakiwa yamemwagika chini.
WATU watano (5) wamenusurika kifo ajalini baada ya gari walilokuwa
wakisafirishia matofali kupasuka tairi la mbele na kuacha barabara kisha
kupinduka.
Ajali hiyo ilitokea jana jioni katika Kijiji cha Ng’ombe wilayani
Misungwi, Mkoani Mwanza ambapo gari hilo aina ya Fuso lenye namba za
usajili T726BMY mali ya Sanne Shimbe, lilikuwa likiendeshwa na tajiri
huyo.
Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo, gari hilo lilikuwa kasi, tairi ikapasuka hivyo gari likapoteza uelekeo na kuacha barabara kisha kupinduka.
Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo, gari hilo lilikuwa kasi, tairi ikapasuka hivyo gari likapoteza uelekeo na kuacha barabara kisha kupinduka.
“Gari lilikuwa kasi hivyo baada ya tairi kupasuka lilitoka barabarani
na kuingia kwenye matuta ya viazi vitamu likakwama ndipo likapinduka,”
alisema shuhuda.
Kwa upande wake dereva Shimbe, alisema baada ya tairi kupasuka alijitahidi kulizuia gari hilo lisianguke lakini ilishindikana.
Kwa upande wake dereva Shimbe, alisema baada ya tairi kupasuka alijitahidi kulizuia gari hilo lisianguke lakini ilishindikana.
“Nilijitahidi kuliweka sawa gari barabarani baada ya tairi kupasuka
lakini ilishindikana kabisa ndio likatoka barabarani na kupinduka lakini
nashukuru Mungu tumetoka wazima.
“Tulikuwa watano, mmoja wetu ndiyo ameumia mguu na ameshapelekwa hospitali, anaendelea vizuri, sisi wengine hatukupata majeraha,” alisema Shimbe.
“Tulikuwa watano, mmoja wetu ndiyo ameumia mguu na ameshapelekwa hospitali, anaendelea vizuri, sisi wengine hatukupata majeraha,” alisema Shimbe.
(PICHA/HABARI: MASHAKA KISUSI, Mwanza)

إرسال تعليق