Jeshi
la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linamshikilia mkazi wa
Mbagala Rangi Tatu, Haroub Mtopa (44) kwa kujifanya mtumishi wa umma
kupitia cheo cha Katibu wa Rais, Jakaya Kikwete, Prosper Mbena.
Kova
aliwaasa wananchi kuepuka kujifanya watumishi wa umma kwani ni kosa
kisheria na kuongeza kuwa wameweka kikosi maalumu kitakachoshughulikia
masuala ya watu wanaozunguka zunguka nje za ofisi za watu pasipo
shughuli maalumu
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu
ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa juzi
jioni.
Kova
alisema Mtopa alikuwa na mazoea ya kujifanya mtumishi wa Ikulu kwa nia
ya kudanganya watu kwamba anaweza kuwasaidia shida zao ili ajipatie
fedha.
Katika
kufanya kazi zake za kitapeli, Kova alisema mtuhumiwa huyo alikuwa
akiingia na kutoka Ikulu mara kwa mara, huku akijifanya kuwa na shida
nyingi hivyo alikuwa akiomba msaada.
‘’Huyu
mtu ni tapeli wa muda mrefu sana, tulimkamata baada ya mwananchi mmoja
kuzungumza na mtuhumiwa huyo na kuahidiana kumpa Sh 500,000 na
kutanguliziwa Sh 250,000. Baadae aliitwa siku nyingine afuate fedha
iliyobaki.
‘’Mwananchi
huyo ambaye hakumtaja jina, alimhofia Mtopa ndipo alipotoa taarifa
Polisi kisha akamwambia mtuhumiwa huyo aende kuchukua fedha iliyobaki,
hatua iliyosaidia Polisi kumkamata kwa urahisi,’’ alisema.
Kova
alisema kuwa mtu huyo ni hatari kwa sababu kutumia cheo cha Katibu wa
Rais inamaanisha kwamba mtu huyo aliweza kutapeli watu wengi sana
kupitia cheo hicho.
Kwa
mujibu wa Kova, mtuhumiwa huyo amekuwa akizunguka katika wizara
mbalimbali ikiwamo ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya
Maji na taasisi nyingine zinazotoa huduma kwa jamii, kwa lengo la
kuomba msaada.
Alisema kabla ya kumkamata, walishirikiana na Ikulu baada ya watu wengi kupeleka malalamiko yao kuhusu mtuhumiwa huyo.

إرسال تعليق