BINTI
aliyefahamika kwa jina moja la Ashura, anayedaiwa kuwa ni mke wa mtu,
hivi karibuni alimtoroka bwana’ke na kuonekana akijiachia hovyo na
wanaume watano tofauti katika Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini
Dar es Salaam kulipokuwa na onyesho la Bendi ya Taarabu ya Mashauzi
Classic.
Ashura, anayedaiwa kuwa ni mke wa mtu akisakata ngoma.
Akionekana kuwa ‘vizuri’
kichwani, kwa kiburudisho alichopata usiku mnene, binti huyo alionyesha
umahiri mkubwa wa kukata mauno kiasi cha kuwavutia wanaume ambao kila
mmoja alitaka kuwa naye karibu kiasi cha kumfanya kuwa bize kwa kila
wimbo kulazimika kucheza na wanaume tofauti.
Hata hivyo baadhi ya mashabiki
wa bendi hiyo walisema mrembo huyo alitia aibu kwani kuna wakati
alicheza hadi nguo zake za ndani zikawa zinaonekana.
إرسال تعليق