Wakizungumza nyumbani kwao jana watoto hao,
walisema baba yao alikuwa akiwatishia kuwakatakata kwa panga au kuwakaba
koo humohumo chumbani endapo wangethubutu kumweleza mtu yeyote kitendo
wanachokifanya.
“Tulikuwa tumeingia kwetu kulala na wadogo zangu,
nikasikia ananiita nikambembeleze mtoto eti anamsumbua, nilikwenda
nikambembeleza akalala, wakati nashuka kitandani kurudi chumbani kwetu
baba akanivuta kwake akanivua, akasema anachokifanya ni suna kwa hiyo
hataki kelele, akisikia atanikaba nife.”
“Niliumia sana na asubuhi mama alirudi
nikajitahidi kweli asijue na hata shule sikwenda, jioni mama aliondoka
tena baba hakuniita siku hiyo lakini baada ya siku tatu aliniita tena
ikawa vilevile navumilia. Siku zilivyozidi unaweza kukuta kwa wiki
naitwa hata mara nne siku ambazo mama hayupo nyumbani,” alisema.
Watoto hao walieleza kuwa baadaye baba huyo
alihamia kwa binti mdogo kwa staili ileile na kila mmoja alikuwa akiitwa
kwa zamu na kwa vile kila mmoja alijua ni siri yake na baba. Kutonaka
na woga wa kuuawa, hakuna aliyemweleza mwenzake hadi katikati ya mwaka
jana mmoja wao alipomweleza mwenzake na baadaye kumweleza mama yao.
“Baba alikuwa anasema atatuua bila hata mtu kujua
na tutaozea shambani, hata nikiwa katika siku zangu baba ananiingilia
hivyohivyo, naugua kila mara UTI, mdogo wangu naye kila mara UTI,
tukaamua liwalo na liwe kama kufa basi ila mama ajue,” alisema mtoto
huyo huku akibubujikwa na machozi.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Miembe Saba,
Hamis Shomari alisema kabla ya kupelekwa kituo cha polisi Kongowe
Jumamosi iliyopita, watoto hao waliitwa shuleni hapo na kuhojiwa kila
mmoja peke yake na wote walikiri kuanza kubakwa mwaka 2013 na baba yao
na kwamba tabia hiyo iliendelea hadi Machi 19 usiku alipobakwa binti
mdogo kwa mara ya mwisho na Machi 20 walipoamua kumweleza mama yao.
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei
alisema wanamshikilia mtuhumiwa huyo na kwamba wasichana hao wamefanyiwa
vipimo mbalimbali na majibu ya daktari yamethibitisha kuwa wamebakwa na
sehemu zao za siri zimeharibiwa, hivyo wanaendelea na matibabu.

إرسال تعليق