Mhe Zitto Zuberi Kabwe
aaga rasmi Bunge...
Mbunge
wa Kigoma Kaskazini Mhe Zitto Zuberi Kabwe usiku huu ametangaza rasmi
Bungeni Dodoma kuachia kiti hicho alichokipata kupitia CHADEMA.
Mhe.
Kabwe ametangaza kung'atuka nafasi hiyo baada ya Mwenyekiti wa Bunge Mhe
Mussa Hassan Zungu Kumruhusu kutoa kauli binafsi mara baada ya wabunge
kumaliza kupitia vifungu vya sheria ya Maafa ambayo hata hivyo
haikupitishwa kwa kutotimia akidi ya wabunge ambao nusu yao hawakuwepo
ukumbini.
Mhe
Zungu alimtakia kila la heri Mbunge huyo machachari ambaye amesema
ameamua kuachia ngazi baada ya chama chake kumfukuza. Hata hivyo
alimalizia kwa kusema kwamba anategemea kuwa nao tena mwezi Novemba
mwaka huu. Hakufafanua. Video ya tamko lake hilo inaandaliwa. Kaa
chonjo..
إرسال تعليق