FISI HAACHIWI BUCHA

He he he heeee, acha nicheke miye mwana Kibatari mjukuu ya Kandili, unajua vitu vingine vinachekesha kama si kusikitisha, unalalamika mwanamke mzima uliyekamilika tena bila aibu eti mfanyakazi wako wa ndani anakulia mali zako kwa mumeo kuhamishia mapenzi kwake!
Unajua kauli hiyo hunifanya nikumbuke ile kauli isemayo mpambe awe mwenye mali na mwenye mali aonekane mpambe. Ooh, nilikuja na kasi ya ajabu na miye bila salamu kwa kuwahi kuzima moto ambao sasa hivi umetanda kila kona ya nyumba zetu hasa wafanyakazi ambao wameolewa na kumuweka msaidizi wa ndani yaani house girl.
Kutokana na kuwa na mfanyakazi wa ndani basi kila kitu unamuachia akifanye, ambacho ni makosa kwa mwanamke aliyefundwa akafundika kumuacha mfanyakazi wa ndani amfanyie mumeo kazi zinazokuhusu!
Tangu lini fisi akaachiwa bucha wewe na mfanyakazi  wako wa ndani mnazidiana nini kimaumbile, pengine mfanyakazi wako Mungu kampendelea kuliko wewe. Kwa vile unafanya kazi basi ukirudi unautupa mkoba wako unakwenda kuoga, ukila unapanda kitandani kutokana na uchovu wa kutwa nzima.
Unamwacha mfanyakazi wa ndani afanye kazi zote kumsubiri mumeo wewe umelala akirudi amtengee maji ya kuoga wewe umelala amtengee  chakula huna habari unajigeuza kitandani. Anaondoa vyombo pengine amevaa upande wa kanga bila kitu ndani  na kama anajua yupo katika mkao wa kula naye hufanya vibweka vya kuchezesha makalio na kuacha matiti nje.
Sehemu hizo ndizo huwatoa imani wanaume na kujikuta akijaribu kwa vile naye ana hamu zake basi shoga wee unalala watu wanajilia vyao. Ulikuwa wa kuamshwa usiku.
“Honey leo nimeshikwa mwenzio.”
Unajikuta unalala kila siku bila kuguswa kutokana na uchovu wa kazi unaona sawa kumbe nyani kaingia shambani wee wapiga usingizi mali zako zinaliwa. Leo na kesho mfanyakazi wako wa ndani anageuka mke mwenzio tena mapenzi yote mumeo anayahamishia kwa mfanyakazi kwa vile ndiye anayemfanyia zaidi ya mke.
Utakalia kulia “Aah, nyani kavamia shamba langu naanza kuvuna mabua,” we mwenyewe umemchekea nyani acha uvune mabua.
Shoga nataka nikueleze sheria za ndoa hata kama unafanya kazi gani hakikisha baadhi ya vitu hasa vimuhusuvyo mumeo mfanyakazi wa ndani havigusi. Kufuliwa nguo, kutengewa maji ya kuoga kula lazima ale mumeo ukiwa pembeni hata kama umeshiba basi mlishane hata tonge mbili.
Mumeo ni lulu isiyotaka kuguswa na mtu, itunze kwa nguvu zako zote, hakikisha hakuna mtu atakayeigusa hata shoga yako ila wewe mwenyewe. Mfanyakazi ana mipaka yake wala asiwe na mazoea kwa mumeo.
Narudia wewe na mfanyakazi hamkupishani kitu kila ulichonacho anacho ana matamanio na yeye vilevile anataka vitu vizuri. Kufanya kazi usijisahau na kuona kazi ni bora kuliko mumeo, kazi ina umuhimu kwa sehemu zake na ukifika nyumbani mwenye nafasi ya pekee ni mumeo, kuhakikisha anapata huduma zote muhimu kutoka kwa mkewe.
Kinachowaumiza wanawake wengi ni uvivu hasa wanapokuwa wanafanya kazi na kumuachia fisi bucha unategemea nini kama siyo kukuta amekula mpaka gogo la kupasulia mifupa.
Yangu nimemaliza, la muhimu kuyafanyia kazi la sivyo utaachika na nyumba unaipenda

Post a Comment

Previous Post Next Post