Jack Patrick, akiwa na mumewe wa ndoa, Abdulatif Fundikira.
Na Waandishi wetu
KATIKA ulimwengu wa wapendanao kuna changamoto nyingi ambazo wapenzi
hukutana nazo huku wengine wakizishinda na baadhi kushindwa.
Wapo wapenzi walioshindwa kuendelea na uhusiano wao mara baada ya
mmoja kuugua, kupata ulemavu na sababu nyingine nyingi, lakini wapo
walioendelea kuvumiliana pamoja na sababu zote hizo na hatimaye penzi
lao likazidi kuimarika na kuwa mfano katika jamii.
Hali hiyo haipo kwa watu wa kawaida peke yao bali hata kwa mastaa
wetu wamejikuta wakiangukia katika mtihani huo na kushindwa kuhimili
kusimamia mapenzi yao. Kifungo au jela ni moja ya sababu zinazosababisha
ndoa au uhusiano wa mastaa wengi na wenza wao kuharibika.
Katika makala haya tunakuletea orodha ya baadhi ya mastaa ambao wamekumbwa na sakata hilo:-
Katika makala haya tunakuletea orodha ya baadhi ya mastaa ambao wamekumbwa na sakata hilo:-
Jack Patrick,
Mumewe na Jux
Jack Patrick ambaye aliwahi kushiriki Shindano la Miss Tanzania 2011, alijikuta akitiwa jela mwishoni mwa mwaka 2013 huko Macao, Hong Kong, China baada ya kudaiwa kukutwa na kete 66 za heroin. Wakati Jack anatumikia kifungo chake mumewe wa ndoa, Abdulatif Fundikira alidaiwa kushindwa kuvumilia na kumuoa kisiri Miss Tanzania 2011, Salha Israel hivyo kuhitimisha rasmi uhusiano wao.

Hata hivyo, wadadavuzi wa mambo walidai kuwa hiyo ilitokana na
malipizi kwa kuwa hata wakati Abdulatif aliposwekwa lupango akihusishwa
na ishu hiyohiyo ya madawa ya kulevya, Jack Patrick naye aliwahi
kumsaliti kwa kutoka na msanii wa Bongo Fleva, Juma Mussa ‘Jux’.
Kajala na Mumewe.
Kajala na Mumewe
Kajala ni staa wa muvi ambaye sakata lake lilianza baada ya yeye na mumewe kuswekwa ndani kwa kosa la kutakatisha fedha na mashtaka mengine. Kajala alitakiwa kutoa faini ya shilingi milioni kumi na tatu (13) au kwenda jela miaka saba (7) huku mumewe, Faraja Chambo akienda jela kutumikia kifungo cha miaka 12 baada ya kushindwa kutoa faini ya shilingi milioni 213. Ashukuruwe Wema Sepetu ambaye alimtoa Kajala kwa kulipa kiasi hicho cha fedha.

Akiwa uraiani, Kajala alidaiwa kushindwa kuvumilia kukaa na upweke na
kukwaa skendo za mapenzi ikidaiwa kutoka na wanaume tofauti lakini
kubwa ni ya kutoka na Kigogo mmoja (jina tunalihifadhi) anayetanua naye
sehemu mbalimbali wakati mumewe akiozea jela bila msaada wowote kutoka
kwake, japokuwa mara kadhaa amekuwa akimuomba Kajala amtoe.
Z. Anto akiwa na aliyekuwa mumewe Sandra.
Binti Kiziwi na Z. Anto
Baada ya kutoka na video ya Wimbo wa Binti Kiziwi, Mbongo Fleva, Z. Anto aliamua kumuoa binti aliyetumika katika video hiyo ‘video queen’ (Sandra Khan).
Baada ya kutoka na video ya Wimbo wa Binti Kiziwi, Mbongo Fleva, Z. Anto aliamua kumuoa binti aliyetumika katika video hiyo ‘video queen’ (Sandra Khan).
Hata hivyo, misukosuko ya ndoa yao ilianza baada ya kutimiza miaka
mitatu ambapo Z. Anto na Sandra walitengana kwa kudai kuwa mkewe alikuwa
akishirikiana na makundi mabaya. Uhusiano wao uliisha rasmi baada ya
Sandra kunaswa mwanzoni mwa mwaka 2013 huko Hong Kong, China akiwa na
‘mzigo’. Katika moja ya mahojiano, Z. Anto alidai kuwa kwa sasa
anaendelea na maisha yake na anatafuta msichana mwingine wa kuoa.
Aunt Ezekiel na Sunday Demonte.
Aunt Ezekiel na Sunday Demonte
Staa wa muvi, Aunt Ezekiel aliwashtusha watu baada ya kuolewa na Sunday Demonte, Mtanzania aishiye ughaibuni.
Staa wa muvi, Aunt Ezekiel aliwashtusha watu baada ya kuolewa na Sunday Demonte, Mtanzania aishiye ughaibuni.
Habari zilidai kuwa mumewe huyo ameswekwa rumande jijini Abu Dhabi
katika nchi za Falme za Kiarabu (UAE) kwa kesi ya madawa ya kulevya.
Kama mastaa wengine, Aunt Ezekiel naye alishindwa kujizuia na kuchepuka
na dansa wa Mbongo Fleva, Diamond Platnumz, Mose Iyobo na hatimaye
kubeba mimba ambayo siyo ya mumewe Sunday.

إرسال تعليق