Muonekano wa mtoto huyo.
WAKAZI wa Mkoa wa Shinyanga wamekumbwa na mshituko
baada ya mama mmoja mwenyeji wa Ndembezi mkoani humo kujifungua mtoto wa
ajabu, Amani limeinasa.
Tukio hilo lilijiri usiku wa kuamkia Machi 12, mwaka huu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Kwa mujibu wa watu waliomwona mtoto huyo waliliambia Amani kwamba, alizaliwa akiwa na masikio yote kwenye shingo, kuanzia kidevuni kwenda kwenye paji la uso vitu vyote vimeangalia juu.
Kwa mujibu wa watu waliomwona mtoto huyo waliliambia Amani kwamba, alizaliwa akiwa na masikio yote kwenye shingo, kuanzia kidevuni kwenda kwenye paji la uso vitu vyote vimeangalia juu.
“Yaani ni mtoto wa ajabu sana. Masikio yapo shingoni. Mdomo, pua na
macho vyote vimeangalia juu mpaka anatisha sana,” kilisema chanzo
kimoja.Kwa mujibu wa chanzo hicho, madaktari wa hospitali hiyo wamekuwa
wakiona akina mama wakijifungua watoto wa ajabu mara kwa mara lakini
wanakiri mtoto huyu wa safari hii ni wa ajabu zaidi kuzaliwa katika
hospitali hiyo.
“Huwezi kuamini ndugu mwandishi jana asubuhi (siku ya tukio) kwenye
vikao vya kawaida vya kila siku hospitalini waliongelea kuzaliwa kwa
mtoto huyo wa ajabu, ujue ni ishu nzito kwao,’’ kilisema chanzo hicho.
Hata
hivyo, mtoto huyo aliishi katika uso wa dunia kwa saa chache na kuaga
dunia huku baadhi ya ndugu wakimtaka mzazi huyo kumshukuru Mungu kwa
kila jambo.
Ilidaiwa kuwa, baada ya mama mzazi kuambiwa hali ya mtoto huyo na
kuoneshwa alibaki kumwaga machozi asijue la akufanya lakini alijipa moyo
na kusema: “Kila jambo hupangwa na Mungu mwenyewe.”
Hata hivyo, baadhi ya wakazi wa eneo hilo walisema kuwa, inabidi kuomba mizimu mara kwa mara ili kuepukana na mikosi kama hiyo.
Hata hivyo, baadhi ya wakazi wa eneo hilo walisema kuwa, inabidi kuomba mizimu mara kwa mara ili kuepukana na mikosi kama hiyo.

إرسال تعليق