Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulraman Kinana akihutubia wakazi wa Itolwa
wilayani Chemba mkoa wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya ziara zake za kujenga
na kuimarisha chama pamoja na kukagua ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2010.

Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Dodoma Alhaji Adam Kimbisa akiwahutubia wakazi wa Itolwa
ambapo aliwaambia kuwa katika chaguzi za mwaka huu hatokata jina la
chaguo la watu.

Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Itolwa wilaya
ya Chemba mkoani Dodoma ikiwa sehemu ya kukagua utekelezaji wa ilani ya
uchaguzi ya CCM 2010.

Wananchi wakifuatilia hotuba za wananchi.

Mbunge wa Jimbo la
Kondoa Kusini Juma Nkamia akiwahutubia wakazi wa Itolwa waliofurika
kuja kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipitia taarifa zinazohusu maji na umeme katika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Chiku Galawa akiwasalimu wananchi wa Itolwa

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa amepata mapokezi makubwa
katika kijiji cha Chandama kata ya Mapango akiwa amaeongozana na Mbunge
wa Jimbo la Kondoa kusini Ndugu Juma Nkamia.

Wananchi wa kijiji cha Chandama wakifurahia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrhaman Kinana.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Songolo

Wananchi
wa kijiji cha Songolo wakimuimbia Katibu Mkuu wa CCMNdugu Abdulrahman
Kinana nyimbo za kumkaribisha katika wilaya ya Chemba.

Wananchi
wa wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye
yupo kwenye ziara ya kukagua ,kuhimiza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi
ambapo katika kata ya Paranga alikagua maendeleo ya ujezi ya wodi ya
mama na mtoto pamoja na kushiriki kupanda miti.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti wa kumbukumbu katika
wodi ya Mama na Mtoto katika zahanati ya Kalema ,kata ya Paranga, wilaya
ya Chemba mkoani Dodoma.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Chemba.

Wajumbe wa Halmashauri Kuu wilaya ya Chemba wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa kijiji
cha Babayu mara baada ya kushiriki ujenzi wa ofisi ya mtendaji.
PICHA ZAIDI
PICHA ZAIDI

إرسال تعليق