KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Simon Sserunkuma.


KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Simon Sserunkuma, amesema kuwa hana furaha na maisha yake kwa sasa ndani ya klabu hiyo na anaomba aruhusiwe atimke.
Kiungo huyo amesema hana furaha kutokana na kuwekwa benchi na kocha Mserbia, Goran Kopunovic.
Nyota huyo aliyesajiliwa wakati wa dirisha dogo msimu huu akitokea Express ya Uganda, amekuwa na maisha magumu kwa sasa kwa kujikuta akikaa benchi kwenye michezo mingi.
Akizungumza na Championi Jumatano, Sserunkuma ambaye ni ndugu wa Dan Sserunkuma ambaye ameshatangaza kutimka, amesema kuwa kwa ujumla hafurahii maisha yake kwa sasa, kwani alikuja kucheza na siyo kuchoma mahindi, maisha ambayo hajayazoea.
Alikwenda mbali na kusema kuwa bado hajaona timu ambayo inamfaa hapa Tanzania kupelekwa kwa mkopo, kwa kile alichosema zote ni ndogo, hivyo angetamani kuangalia mbele zaidi.“Binafsi sina furaha kwa kifupi, kwanza nilikuja huku kucheza mpira na siyo kukaa benchi na walinihakikishia hilo wakati nakuja, lakini pia mimi nimechezea katika timu nyingi tena kubwa, sijawahi kukutana na maisha kama haya.
“Of course’ ni lazima niumie maana nitakuwa najiharibia mwenyewe kipaji, ni bora nipate sehemu ambayo ninaamini nitapata uhakika wa kucheza,” alisema kiungo huyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post