Najua umenisubiri kwa hamu kubwa bi shosti, ni mimi yuleyule mtambo
wa kurekebisha tabia nimeingia kama upepo wa kimbunga. Kwa vile nia ya
kona hii ni kutibu si kubembeleza watu wala kuangalia sura zao. Unajua
kuna baadhi ya wanawake wanatia kichefuchefu kufanya utani katika ndoa
na kuzifanya ndoa za siku hizi zipoteze maana na kushindwa kutofautisha
yupi kaolewa na yupi kahaba.
Nimebahatika kuhudhuria kicheni pati nyingi nikiwa kama mgeni
mwalikwa, nashukuru Mungu kila aliyenialika alikubali ushauri wangu.
Siku zote nimekuwa nikiwaeleza kuwa anayejua ladha ya kitu ni yule
aliyekionja hata akikielezea atakielezea kwa ufasaha zaidi tofauti na
yule asiyeijua ladha atabahatisha kwa vile alisikia tu muonjaji
akielezea utamu na uchungu wa kitu kile.
Kwa kweli bado nalia na maadili mabaya katika ndoa za watoto wetu wa
karne hii, wewe mzazi unaalika watu kuja kumfunda mwari wakiwa hawajui
nini maana ya ndoa kwa vile wamesikia basi ndiyo wanatoa mafundisho
kwamba ndoa inatakiwa hiki na hiki, kwa kukisikia na si kwa uhalisia
ndiyo maana wanakaa uchi mbele ya mwari sasa wamekuja kumfundisha mema
au maovu?
Leo nataka kuzungumza na kina mama wakosa haya wasiyojua vibaya,
inawezekana kabisa ndoa yako inawaka moto kutokana na ujinga wako kiburi
kujisikia humjali mume unataka kila kitu ukipate usipopata mumeo humpi
haki ya ndoa. Leo hii wewe unamcheza mwanao na kuwaita wakosa haya
wenzako mje mumfunde mwari.
Mtamfundisha nini kama siyo wewe kuwa chanzo cha kuiharibu ndoa ya
mwanao? Hao mashoga zako wanatoa nasaha za aibu mbele ya binti yako
anayetaka kuolewa nawe upo pembeni unapiga vigelegele mtoto kaolewa
kesho kaachika mbaya nani?
Japokuwa kicheni pati si sehemu sahihi ya kumfunda mwari, basi
tutafute watu waliodumu kwenye ndoa zao kwa muda mrefu ili waweze kutoa
nasaha halisia wala si za kuhisia. Hata mavazi yao ni somo tosha kwa
mwanao kuonesha mwanamke anatakiwa kustiri maungo yake kwa vile mhusika
wa kuyaona ni mumewe tu.
Mbele unamsimamisha mwanamke mwenye sifa ya kuchanganya wanaume kama zege nguo alizovaa mwili wote upo nje na yeye anakueleza eti ndoa ni ngumu mheshimu mumeo. Wakati yeye pengine ameachika ndoa zaidi ya tatu.
Mbele unamsimamisha mwanamke mwenye sifa ya kuchanganya wanaume kama zege nguo alizovaa mwili wote upo nje na yeye anakueleza eti ndoa ni ngumu mheshimu mumeo. Wakati yeye pengine ameachika ndoa zaidi ya tatu.
Siku zote mfano mzuri ni wa vitendo si wa maneno, anayekufunda
ukimuangalia kweli anachokisema ndicho anachokifanya. Kwako unamchukulia
kama mfano wako katika maisha ya ndoa, ili ukiteleza basi umkimbilie
mara moja kukupa mungozo wa ndoa yako ili ujue umejikwaa wapi na ufanye
nini.
Kingine wazazi sisi ndiyo tunatakiwa kuwa viongozi wa watoto wetu
waipende ndoa kupitia maisha yetu ya ndani ya wewe na mumeo. Ndani ya
nyumba hamzungumzi au mama anamdharau baba. Pale unamfundisha nini
mwanao ina maana na yeye atajua kumbe kumdharau mwanaume ni jambo la
kawaida na ni haki ya msingi.
Kama kweli tuna nia nzuri na watoto wetu basi sisi ndiyo walimu wa
kwanza kuhakikisha ndoa zao zinadumu. Tujiepushe kuwashirikisha watu
wasiojua thamani ya ndoa, kila aliyeionja ndoa ataielezea kwa ufasaha
zaidi ili muolewaji basi apate faida na kujiandaa vizuri katika ndoa
yake.
Wazo langu jipya ambalo najua litakushtua lakini kama wazazi
mtalifanya hili basi nina imani watoto wenu wa kike watapata faida kubwa
katika ndoa zao.
Muda ukikaribia mtoto wako wa kike kuolewa kama hakupitia unyago
mweke chini ukiwa na shoga zako waliodumu kwenye ndoa zao kwa muda mrefu
mwelezeni ndoa ni nini, utamu na uchungu wa ndoa ambao wote umebebwa na
upendo, heshima, adabu, huruma na uvumilivu.
Nina imani somo hili likifanyiwa kazi, tutafanya ndoa zipate heshima kuliko kuwaita wahuni kutukana mbele yamwari wetu. Yangu leo yanatosha tukutane wiki ijayo.
Nina imani somo hili likifanyiwa kazi, tutafanya ndoa zipate heshima kuliko kuwaita wahuni kutukana mbele yamwari wetu. Yangu leo yanatosha tukutane wiki ijayo.

Post a Comment