BARAZA
la kiislam nchini (BAKWATA) limewataka waamini wote wa dini ya kiislam
nchini kuisoma Katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba ili
kuielewa na kuipigia kura ifikapo tarehe 30-april kwaka huu.
Kauli
hiyo ya BAKWATA inakwenda tofauti na Mwamvuli wa Jukwaa la Wakristo
Tanzania, ambalo ni pamoja la Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania
(TEC), Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) na Baraza la Makanisa ya
Kipentekoste Tanzania (CPCT) ambao wao walitoa tamko ambalo limesomwa
kila kanisa wiki hii, likiwataka waamini wa dini ya kikristo kupigia
kura ya Hapana katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba.
Mbali
na maaskofu, Bakwata wamekwenda tofauti na Jumuiya ya Taasisi za
kiislam nchini ambao nao wamewataka pia waamini wa dini hiyo kupigia
kura ya hapana katiba hiyo kama haitoitambua Mahakama ya Kadhi.
Kauli
ya Bakwata imetolewa Leo jijini Dar es Salaam,na Mkuu wa Bakwata mkoa
wa Dar es Salaam Sheikh Alhad Mussa Salum wakati wa Mkutano na Waandishi
Habari pamoja na mambo mengine amesema kwa sasa wao Bakwata hawezi
kuwataka waislam nchini kuipigia kura ya hapana katiba iliyopendekezwa
na Bunge Maalum la Katiba.
"Sisi
tumewataka waamini wa dini ya kiislam nchini kuisoma kwa umakini katiba
iliyopendekwa na Bunge maalum la Katiba na ikifika wakati wa kupigia
kura waamue wenyewe,maana sisi hatuwezi kuwalazimisha kupigia kura ya hapana kama wanavyofanya wengine”amesema Sheikh Salum.
Katika
hatua nyingine Sheikh Salum ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Amani
,amemvaa katibu mkuu wa chama cha mapinduzi CCM,Mh Abdurahman Kinana
kutokana na kitendo chake cha kumshambulia Waziri wa Maliasili na
Utalii Lazaro Nyalandu kwa kumwita waziri huyo ni mzurulaji na wala
hafanyi kazi yoyote na kwamba anathamini wanyama kuliko binadamu
“Kamati
ya amani imesikitishwa sana na kauli za Kinana ambazo zinalenga
kumbeza waziri Nyalandu katika jitihada zake anazochukua katika
kupambana na majangili wa wanyama ambao wamekuwa wakimaliza wanyama” Ameendelea kusema Sheikh Salum.
Aidha
Sheikh Salum amemtaka katibu huyo wa CCM kuacha kumbeza Waziri Nyalandu
na akamtaka kuwaangalia wakuu wa Wilaya pamoja na Mikoa ambao wamekuwa
na tabia ya kuzurula bila kuwa na mipango yoyote.
إرسال تعليق