Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mohamed Thabit Kombo akimpongeza Mwenyekiti wa Mfuko huo,Doris Mollel kwa kuona jukumu la kusaidia jamii katika kuokoa maisha ya watoto njiti. |
Naibu
Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mohamed Thabit Kombo
akizungumza wakati wa hafla ya kutambulisha Mfuko wa Doris
Mollel,iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency,jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti
wa Mfuko huo,Doris Mollel akizungumza na wageni waalikwa waliofika
kwenye hafla ya kutambulisha Mfuko wa Doris Mollel,uliofanyika kwenye
Hoteli ya Hyatt Regency,jijini Dar es salaam.
Naibu
Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mohamed Thabit Kombo
(pili kushoto),Balozi Mwanaid Maajar (kulia),Mwenyekiti wa Mfuko
huo,Doris Mollel (katikati) pamoja na wadau wengine wa Mfuko huo
wakishiriki kwa pamoja kukata keki,kuashiria uzinduzi rasmi wa Mfuko wa
Doris Mollel,uliofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency,jijini Dar es
salaam.
Sehemu
ya Wageni waalikwa katika hafla ya kutambulisha Mfuko wa Doris
Mollel,iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency,jijini Dar es salaam.
Mrembo wa singida aliyeshika nafasi ya tatu katika mashindano ya miss tanzania mwaka wa
2014 DORIS MOLEL leo amezindua rasmi rasmi DORIS MOLEL foundation ambayo ni
mahususi kwa ajili ya kusaidia watoto ambao wamekuwa wanazaliwa wakiwa bado hawajatimia
NJITI ambapo amewataka watu mbalimbali kujitokeza kumpa saport katika shighuli
hiyo.
Uzinduzi huo ambao
umefanyika leo jijini dare s salaam na kuhudhuriwa na viongozi pamoja na wadau
wanaohusika katika kuwasaidia watoto hao wengi wamepongeza jitihada zinazoonyeshwa na
mrembo huyo kwani watoto wanaozaliwa wakiwa na tatizo hilo wamekuwa
wakusahaulika sana nchini tanzania jambo ambalo limetajwa kuwaadhiri watoto hao
pamoja na wazazi wao.
Mrembo DORIS ambaye nayeye
ni mmoja kati ya watu walioadhirika na
tatizo hilo alizaliwa akiwa njiti akizungumza katika uzinduzi huo amesema kuwa
ameamua kuwasaidia watoto na wazazi wenye matatizo hayo baada ya yeye kupitia katika
kipindi kama hicho ambapo amesema kinahitaji msaada mkubwa kutoka kwa watu wa
karibu.
“Mimi nilizaliwa nikiwa
njiti nilikuwa sijafikisha uzito halali wa kuzaliwa lakini nilizaliwa na mama
akanisaidia hadi leo hii mnaniona hapa ni miss Tanzania na ni mtu nayekubalika
na jamii,hivyo nimeona kuna haja ya kuwasaidia watoto kama mimi ambao wamezaliwa
hivyo ili waweze kukua na afya njema na baadaye kutimiza malengo ya maisha
yao”alisema mrembo huyo.
Amesema kuwa baada ya
kuchaguliwa ,kuwa mrembo namba tatu wa Tanzania alifikiria kitu cha kufanya ili
arudishe shukrani kwa watanzania na baada ya kutembea katika maeneo mbalimbali
aligundua kuwa watoto wanaokumbwa na matatizo hayo bado wamekuwa hawapewi
kipaumbele katika kusaidiwa jambo ambalo limemsukuma yeye kuanza kufanya
mchakato huo.
Aidha amesema kuwa ipo
haja ya serikali pamoja na wadau mbalimbali kuunga mkono jitihada hizo kwa
lengo la kuokoa kizazi kikubwa ambacho kinazaliwa na matatizo kama hayo ambapo
kwa takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya watoto laki mbili wanazaliwa wakiwa njiti kwa
mwaka nchini Tanzania.
Uzinduzi huo ulienda
sambamba na uchangiaji wa fuko huo kwa ajili ya kuwasaidia watoto hao ambapo
watu mbalimbali walijitoa kuchangia mfuko huo na kuwaomba watanzania wengine
kuendelea kumsaidia mrembo huyo kuhakikisha kuwa anatimiza lengo lake.
Baadhi ya watu
waliojitokeza kumpa nguvu katika shughuli hiyo leo ni pamoja na muandaaji wa
mashindani ya miss tanzania ambapo ndiko mrembo huyo alikotokea bwana hashimu
lundenga,mwenyekiti mstaafu wa bodi ya usafiri dare s salaam UDA mzee iddi
samba,Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mohamed Thabit Kombo pamoja na viongozi mbalimbali kutoka bara na Zanzibar.
إرسال تعليق