Mtangazaji wa ITV na redio, Salma Dakota hivi karibuni alipoteza
fahamu baada ya kufanyiwa ‘sapraizi’ ya kuvishwa pete ya uchumba na
mpenzi wake, Gharibu Dumba.
Ilielezwa kuwa, Salma akiwa hana hili wala lile, alishangaa akivishwa pete ya dhahabu yenye kito cha Tanzanite ambayo gharama yake ni takriban shilingi milioni 3.
Salma Dakota Akionyeshwa pete aliyovishwa.
Tukio hilo lilitokea kwenye Hoteli ya Protea iliyopo jijini Dar es
Salaam ambapo alikwenda bila kujua kuwa mtu wake huyo alikuwa na jambo
kubwa la kumfanyia.Ilielezwa kuwa, Salma akiwa hana hili wala lile, alishangaa akivishwa pete ya dhahabu yenye kito cha Tanzanite ambayo gharama yake ni takriban shilingi milioni 3.
Mtangazaji wa ITV na redio, Salma Dakota akiwa kwenye pozi.
Akizungumzia tukio hilo mtangazaji huyo alisema: “Nilipata mshituko
kwani sikutarajia na ndiyo maana nikapatwa na hali ile. Namshukuru Mungu
kwa hili lililonitokea, ni jambo la heri na Mungu aniongoze katika
safari hii ya kuelekea kwenye maisha ya ndoa.”
إرسال تعليق