MWANAMKE
mmoja mwenye asili ya Kiarabu, Salma Amuri (39) (pichani) mkazi wa Mji
Mpya, Kawe jijini Dar, amenusurika kifo baada ya kuchomwa visu sehemu
mbalimbali za mwili wake ikiwemo tumboni na mumewe aliyetambulika kwa
jina moja la Selemani.Mwanaume huyo naye baada ya tukio hilo alijaribu
kujiua kwa kunywa sumu, chanzo kikidaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Salma Amuri anayedaiwa kuchomwa visu na mumewe akiwa hoi hospitalini.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa chanzo chetu, tukio hilo lilitokea
saa saba usiku wa kuamkia Alhamisi iliyopita ambapo mwanamke huyo
alijeruhiwa vibaya kiasi cha kufanya utumbo wake kutoka nje, kabla ya
ndugu na wasamaria wema kuwachukua wawili hao na kuwakimbiza Hospitali
ya Mwananyamala, wote wakiwa mahututi.
Gazeti hili lilizungumza na mwanamke huyo hospitali ambapo alieleza kisa cha tukio hilo.
Gazeti hili lilizungumza na mwanamke huyo hospitali ambapo alieleza kisa cha tukio hilo.
“Migogoro ndani ya ndoa yetu tuliyofunga miaka ishirini iliyopita na
kufanikiwa kupata watoto na wajukuu, ilianza tangu Novemba, mwaka jana
baada ya kutembelewa na ndugu yangu aliyekuja Tanzania akitokea Saudi
Arabia anakoishi.
“Mume wangu alikuwa ananishutumu kwamba ameambiwa na majirani mimi
natembea na huyo mtoto wa mama yangu mdogo, jambo ambalo siyo la kweli
kwani hata kiumri, ni mdogo, hajafikisha hata miaka thelathini,” alisema
mwanamke huyo.
Moja ya jeraha alolipata mwilini mwake.
“Usiku siku ya tukio saa saba usiku alirudi nyumbani akawa amekaa
sebuleni lakini baada ya kumtaka twende tukalale aligoma, mimi nikarudi
ndani, mara akaja na kuniambia ameamua kujiua huku akinionesha sumu
aliyokuwa ameiandaa kwenye chupa ili anywe.”Aliongeza kuwa alivamiwa
ghafla na kushambuliwa kwa kisu kisha alipoteza fahamu akajishitukia
akiwa pale hospitali.
Jitihada za kumsikia mumewe ambaye awali naye alikuwa amelazwa kwenye
hospitali hiyo, ziligonga mwamba kwa kuwa alikuwa amelazwa chini ya
ulinzi wa polisi.Kamanda wa Polisi Kanda ya Kinondoni, jijini Dar, ACP
Camillius Wambura alikiri kutokea kwa tukio hilo. “Mumewe alihamishiwa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na hali yake kuwa mbaya na
mwanamke yupo Mwananyamala, uchunguzi bado unaendelea,” alisema Wambura
Post a Comment