Mwimba Injili, Victor Mwailenge (29) ambaye ni mkazi wa Mtaa wa
Migombani,Tunduma, Wilaya ya Momba mkoani Mbeya, Machi 17, mwaka huu
anadai kukumbwa na majeraha makubwa mkononi yaliyotokana na mlipuko wa
bomu lililotupwa na polisi katika vurugu baina ya askari na wananchi.Mwimba Injili, Victor Mwailenge akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa na bomu.
Kijana huyo aliliambia Uwazi juzi katika mahojiano kwa njia ya simu
ya kiganjani kuwa, wakati vurugu hizo zikitokea kutokana na mgogoro wa
ardhi wiki iliyopita alivuka mpaka na kuingia nchini Zambia na
kujihifadhi katika duka la rafiki yake ndipo bomu lililorushwa na askari
lilimfuata huko.
Majeruhi huyo ambaye anaimba nyimbo za Injili katika Kanisa la
Moravian alikuwa na haya ya kusema juu ya mkasa uliompata:“Saa 10.30
alfajiri nikiwa maeneo ya Black Market, mpakani mwa Tanzania na Zambia
kutokana na vurugu nililazimika kuvuka mpaka kwani mimi nilikuwa
sihusiki katika vurugu hizo, nilitarajia kwamba zikiisha nivuke mpaka
nirudi nyumbani Tunduma,” alisema kijana huyo.
Muonekano wa jeraha alolipata baada ya kulipukiwa na bomu hilo.
Alipoulizwa sababu za vurugu hizo alisema: “Kisa ni mgogoro wa ardhi,
wananchi wanataka eneo hilo la Sogea liwe la shughuli za kijamii kama
soko, kupaki magari na kujengwa hospitali lakini CCM nao wanasema ni
lao.
“Lakini pia yupo mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina moja la mama Komba naye alidai kuwa ni eneo lake na kwamba ana hati, alienda mahakamani akaambiwa aende baraza la usuluhishi la ardhi kata ili haki ipatikane.
“Lakini pia yupo mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina moja la mama Komba naye alidai kuwa ni eneo lake na kwamba ana hati, alienda mahakamani akaambiwa aende baraza la usuluhishi la ardhi kata ili haki ipatikane.
“Kabla ya ufumbuzi kupatikana viongozi waliwaambia wananchi kuchimba
msingi ili wajenge zahanati, polisi walifika katika eneo hilo na
kusitisha zoezi hilo, waligoma kutawanyika ndipo walitawanywa kwa nguvu
kwa kutumia mabomu, hasira ziliwapata hali iliyowafanya wajibu mapigo.
“Polisi hao walidaiwa kumpiga Diwani wa Kata ya Tunduma, Frank
Mwakajoka hali iliyoamsha hasira kwa wananchi, ghasia ziliongezeka.
“Siku ya pili kila moja alifungua duka, ghafla tulishangaa kuona polisi,
vurugu zikaanza upya na polisi kurusha mabomu ndipo moja lilinipata
nikalidaka na kunilipukia mkononi.
“Kwa
sasa siwezi kufanya kazi yoyote na anahitaji msaada kwani nina mke na
watoto wanne wanaomtegemea.” Aliyeguswa na habari ya Victor anaweza
kuwasiliana naye kwa simu namba 0752 339 274.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya SACP, Ahmed Msangi alipoulizwa alisema ni kweli vurugu hizo zilitokea, “Hivi sasa watu 26 walikamatwa kutokana na hilo,” alisema.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya SACP, Ahmed Msangi alipoulizwa alisema ni kweli vurugu hizo zilitokea, “Hivi sasa watu 26 walikamatwa kutokana na hilo,” alisema.
Post a Comment