USHIRIKINA? Katika hali ya kushangaza, Wilson Saimon ‘Babu Nyemeni’ (21), mkazi wa Kijiji cha Mgeta wilayani Mvomero mkoani Morogoro yamemkuta baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kudaiwa kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka mitatu.
Babu Nyemeni anadaiwa kufanya unyama huo mwishoni mwa mwaka jana,
nyumbani kwa Angel Bosco ambaye alikuwa amekwenda kuimba kwaya kanisani
na kumuacha nyumbani mtoto huyo (jina tunalihifadhi) akiwa na mfanyakazi
wake wa ndani.
Akisoma hukumu ya kesi hiyo katika Mahakama ya Wilaya ya Morogoro,
Hakimu Mkazi, Regina Futakamba alisema siku ya tukio mtuhumiwa huyo
ambaye ni jirani yake Angel, alimuomba mtoto huyo kwa mfanyakazi wa
ndani na kumwambia anakwenda kumnunulia pipi, mfanyakazi alimkubalia
ndipo alipokwenda kumbaka kichakani, jambo ambalo mtuhumiwa huyo
alilikiri mahakamani.
Alisema mtoto huyo alikutwa katika kichaka kilicho nje kidogo ya
kijiji hicho akiwa analia kwa maumivu ndipo walipompeleka kwenye
Zahanati ya Mgeta alikobainika alibakwa na kuharibiwa sehemu za siri.
Hakimu Regina alisema kutokana na kosa hilo, mtuhumiwa alitakiwa kufungwa kifungo cha maisha lakini alitoa nafasi kwa mtuhumiwa kujitetea ambapo alijitetea na hakimu kumpunguzia adhabu hiyo kwa kumfunga miaka 30 jela ili iwe fundisho kwa wengine.

Wakizungumzia tukio hilo, baadhi ya wananchi wa Mgeta walilihusishwa
tukio hilo na imani za kishirikina kwani walisema walishangazwa na
mtuhumiwa kumbaka mtoto mdogo kiasi hicho.
“Mh! Hii nahisi inawezekana kadanganywa na waganga kwamba atembee na mtoto mdogo ndiyo apate utajiri maana haya mambo nayo yapo,” alisema mkazi mmoja wa Kijiji cha Mgeta.
“Mh! Hii nahisi inawezekana kadanganywa na waganga kwamba atembee na mtoto mdogo ndiyo apate utajiri maana haya mambo nayo yapo,” alisema mkazi mmoja wa Kijiji cha Mgeta.
إرسال تعليق