BEKI Joseph Owino na mshambuliaji Ramadhan Singano ‘Messi’
wamereja kikosini Simba baada ya kujiunga na wenzao kwenye kambi ya
mazoezi kujiandaa na mechi yao na Kagera Sugar.
Owino na Singano walikuwa hatarini kukosa mechi
hiyo kutokana na kusumbuliwa na malaria, lakini Daktari wa timu hiyo,
Yassin Gembe amethibitisha uimara wa afya za wachezaji hao na kwamba
watakuwa kwenye mechi hiyo ya Jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa Kambarage,
Shinyanga.
Gembe aliliambia Mwanaspoti kuwa wachezaji hao
akiwemo Ivo ambaye ataikosa mechi hiyo kwa kadi nyekundu aliyoonyeshwa
dhidi ya Mgambo JKT, wataanza mazoezi ya wenzao leo kwenye Uwanja wa
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya makocha wao Goran Kopunovic na
msaidizi wake Seleman Matola
“Owino na Singano wanaendelea vizuri na wataanza
mazoezi kesho (leo) Jumatatu, hata mechi yetu na Kagera wanaweza
kucheza, naamini watakuwa wapo vizuri zaidi, walikuwa wakisumbuliwa na
malaria lakini hivi sasa wamepona,” alisema Gembe.
Kwa upande wa Owino aliliambia Mwanaspoti kuwa:
“Nipo vizuri kwa maana ya kwamba nimepona, kuhusu mechi hiyo itategemea
na kocha atakavyoamua, kwa sasa mimi namsikiliza kocha anavyopanga
kikosi chake cha kwanza na wachezaji watakaoanzia benchi.”
Tangu mzunguko huu uanze wa Ligi Kuu Bara, Owino
hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara kutokana na nafasi yake
kuchukuliwa na Juuko Murshid ambaye pia ni raia wa Uganda.
Owino amecheza mechi moja na nyingine alianzia benchi huku hatima yake Simba ikiacha maswali
Post a Comment