Jumapili
iliyopita mkurugenzi wa Mashauzi Classic, Isha Mashauzi alikwea jukwaa
la Jahazi Modern Taarab na kuleta msisimko wa aina yake.
Isha
ni msanii aliyechipuka na kuwa maarufu kupitia Jahazi Modern Taarab
kabla hajaamua kuanzisha bendi yake miaka minne iliyopita.
Mara
tu Isha alipopanda jukwaani sambamba na Mzee Yussuf mashabiki
wakalipuka kwa furaha na kukumbukia vitu vyake adimu alivyovifanya ndani
ya kundi hilo.
Isha
alitumia muda wake jukwaani kunadi onyesho la pamoja la Jahazi na
Mashauzi litakalofanyika Travertine Hotel Magomeni Jumapili ya tarehe 22
mwezi huu.
Akawapa vionjo vifupi vifupi vya nyimbo zake kadhaa ukiwemo “Yawenzenu Midomoni” aliouimba akiwa na Jahazi.
Mashabiki
wakalipuka kwa furaha na kumtaka aimbe wimbo huo lakini yeye na Mzee
Yussuf wakawaambia mashabiki hao wavute subira na wasipunguze utamu wa
Machi 22.

Mzee Yussuf (kushoto) akisisitiza jambo na Isha Mashauzi (katikati)

Isha akipagawisha kwa vionjo vyake

Shabiki akienda mtunza Isha jukwaani

Mtu na mwanae walivyopendeza jukwaani

Baada ya kushuka jukwaani bado Isha na Mzee waliendelea kujadiliana mambo kadha wa kadha

Mjadala wa hapa na pale ukiendelea

إرسال تعليق