Sauti
ya Kada wa CCM, aliyekuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi na Kiongozi wa
Kikundi cha Tanzania One Theatre (TOT), Kapteni John Komba, huenda
ikaendelea kusikika katika vibao vipya ambavyo alishaviandaa.
Alisisitiza
kuwa pamoja na Serikali kulinda uhuru wa habari, lakini ni lazima iwe
makini kwa kuwa uhuru huo ukitumika vibaya, una madhara kwa jamii
Akizungumzia
msiba huo, katika mahojiano ya ana kwa ana na Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu
wa Azam Media, Tido Mhando, Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya
Kikwete alisema Komba alikuwa akifuatilia malipo ya kusanifu nyimbo za
kampeni.
Alisema
kabla ya Kapteni Komba kufikwa na mauti, Jumamosi iliyopita ya Februari
28, mwaka huu, asubuhi yake alituma ujumbe mfupi wa maandishi wa simu
ya mkononi, kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akimshukuru kwa
kupokea fedha kwa ajili ya kusanifu nyimbo hizo.
Rais
Kikwete aliyekuwa akizindua studio za kisasa za Azam Media, alisema
siku hiyo walipokuwa katika kikao cha Kamati Kuu ya CCM, alipokea ujumbe
kuhusu msiba huo, akamuonesha Kinana ambaye alijikuta akisema;
“haiwezekani.”
Alisema
Kinana alimwambia kwamba asubuhi ya siku hiyo, aliwasiliana na Kapteni
Komba, ambaye alimshukuru kwa kupokea fedha hizo za kusanifu nyimbo hizo
katika akaunti ya TOT.
“Kifo
hiki kimetushitusha kwa sababu alikuwa hajaugua muda mrefu. Tumezoea
mgonjwa unakuwa naye muda mrefu, anakusumbua mpaka unakuwa na wasiwasi
kuwa kesho anaweza asiwepo, lakini hilo halikutokea kwa Komba.
“Asubuhi
aliwasiliana na Kinana, alikuwa akifuatilia malipo ya fedha za TOT kwa
ajili ya kufanya usanifu wa nyimbo za kampeni. Alipopata malipo akampa
taarifa Kinana asubuhi kuwa fedha zimeshafika,” alisema.
Mwili
wa Komba uliagwa jijini Dar es Salaam Jumatatu ya wiki hii katika
viwanja vya Karimjee, ambapo nyimbo zake zilisababisha majonzi makubwa
kwa waombolezaji.
Moja
ya nyimbo hizo, ni pamoja na ule alioimba katika msiba wa Baba wa
Taifa, Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1999, ambao ulipopigwa uliibua
majonzi na kusababisha viongozi mbalimbali, akiwamo Rais Kikwete, kutoa
machozi.
Wimbo
huo uliobadilishwa maneno yaliyomhusu Mwalimu Nyerere na kuingizwa
yaliyomtaja mbunge huyo wa Mbinga Magharibi, ambapo mbali na Rais
Kikwete, ulimliza pia Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, Spika wa Bunge,
Anne Makinda, Mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka, Katibu Mkuu
mstaafu wa CCM, Yusuf Makamba na waombolezaji wengine.
Sehemu
ya mashairi ya wimbo huo uliokwenda kwa jina la 'Nani Yule' ulioimbwa
na wanamuziki mbalimbali wa bendi nchini, na kuwatoa watu machozi
uliimbwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye.
“Kapteni
Komba familia yako umeiacha na nani, chama chako umekiacha na nani,
nenda baba msalimie Mwalimu, mweleze hali ya Watanzania ilivyo hivi
sasa, mweleze hali ya nchi yetu ilivyo hivi sasa hasa wakati huu,
msalimie Mzee Kawawa Simba wa Vita.”
Komba aliyekuwa na miaka 61, alizikwa kijijini kwake Lituhi, wilayani Nyasa Jumanne Machi 3, mwaka huu.
Katika
hatua nyingine, Rais Kikwete ameelezea kutokasirishwa na utendaji wa
vyombo vya habari katika uibuaji wa ubadhirifu serikalini, ikiwemo
katika sakata la kampuni ya ufuaji umeme wa Richmond na utoaji wa fedha
katika iliyokuwa akaunti ya Tegeta Escrow, katika Benki Kuu (BoT).
Akijibu
swali la Mhando kuhusu Serikali kuonekana kukasirishwa na vyombo vya
habari kuibua maovu, Rais Kikwete alisema hilo hana shida nalo,
isipokuwa kunapotokea uchochezi, haitavumilika.
Alitoa
mfano wa mauaji ya Kenya na ya kimbari ya Rwanda, ambayo alisema katika
matukio hayo yaliyokuwa na athari katika jamii, waandishi wa habari
walihusishwa.
إرسال تعليق