Kuna njia mbalimbali za uzazi wa mpango na kila ya uzuiaji mimba
ina faida zake na hasara. Hata hivyo kuna chaguo mbalimbali ambazo
zinafanya kazi kwa kila mwanamke au mwanaume.
Daktari au muuguzi aliyefunzwa uzazi wa mpango
anaweza kumsaidia kila anayehitaji huduma kuamua ni njia ipi sahihi
kwake kwa muda mrefu.
Afya ya uzazi ni ya msingi kwa afya ya ujumla na
ustawi wa mtu mmoja mmoja, wana ndoa, familia na kwa maendeleo ya
kijamii na kiuchumi.
Shirika la Afya Duniani (WHO) limekuwa
likisisitiza njia za uzazi wa mpango zinazozingatia afya ya uzazi kwa
maana kwamba hali ya kuwa mkamilifu kimaumbile, kiakili na ustawi wa
kijamii kwa mambo yote yanayohusiana na mfumo mzima wa uzazi.
Kwa hiyo, afya ya uzazi inamaanisha kwamba watu
wanaweza kuwa na maisha ya kujamiina yanayojitosheleza na salama na
kwamba wanaweza kuzaliana na kuwa uhuru katika kuamua mambo
yanayowahusu.
Ndiyo maana njia mbalimbali za uzazi wa mpango zimefanyiwa tafiti za muda mrefu ili kuthibitisha usalama wake kwa mtumiaji.
Zipo aina nyingi za uzazi wa mpango miongoni ni
zile zinazomhusu mwanamke kama vile kutumia kalenda, kumeza vidonge,
kuchoma sindano au vipandikizi.
Pia zipo njia ambazo zinaweza kuwahusisha pande zote, mwanaume na mwanamke, kama vile kondomu na kufunga uzazi.
Kufunga uzazi kunaweza kutekelezwa na wanandoa kwa maana kwamba hawatarajii tena kuendelea kuzaa.
Kama mpango huu ukitekelezwa kwa mwanamke ina maana kwamba mirija inayopeleka yai kwenye kizazi, huzibwa kabisa.
Vivyo hivyo kwa wanaume, mirija inayotoka kiwandani kupeleka mbegu tayari kutoka na kurutubisha yai, hukatwa na kufungwa.

إرسال تعليق