STAA wa sinema asiyekaukiwa matukio Bongo, Wema
Sepetu amezua kioja cha aina yake baada ya kutajiwa jina la aliyekuwa
mwandani wake, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Staa wa sinema asiyekaukiwa matukio Bongo, Wema Sepetu.
Kioja hicho alikifanya juzikati nyumbani kwake, Kijitonyama jiji Dar
alipokuwa akirekodi kipindi chake cha In My Shoes ndipo aliposhtuka
baada kutumiwa maoni na moja wa shabiki wake kupitia mtandao wa
simu.“Heeeh! Huyu vipi tena ananitajia jina hili (Diamond)? Sitaki
kabisa kulisikia, hapa nataka kusikia mimi na maisha yangu na si maisha
ya mtu mwingine,” alisikika Wema.
إرسال تعليق