Ajali ya Hiace huko Tukuyu Mbeya: Abiria zaidi ya 20 wapoteza maisha, Utingo pekee anusurika

Baadhi ya miili ya walipoteza maisha kwenye ajali ya gari aina ya Hiace iliyopinduka Mtoni, ikiwa imefunikwa baada ya kuopolewa na wasamaria wema huko,  eneo la Uwanja wa Ndege, Kiwira Kyela.
Na Andrew Chale wa Modewji blog
“Tuamke na Mungu, tutembee na Mungu. Hivi ndivyo tunavyoweza kusema kwa sasa kufuatia hali ya ajali za mara kwa mara zinazotokea ndani ya nchi yetu”.
Asubuhi ya leo huko Tukuyu Mkoani Mbeya imeripotiwa ajali mbaya ya Hiace iliyoua takribani watu zaidi ya 20, eneo la Uwanja wa ndege Kiwila Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya.
Imeelezwa kuwa, miili 22 imefanikiwa kutolewa baada ya Hiace hiyo  iliyotumbukia mtoni na bado miili miwili imenaswa, huku ikielezwa kuwa watu wawili tu ndio wamepona akiwemo kondakta.
Ilielezwa kuwa,  Ajali imetokea wakati Coaster zinazofanya safari zake kati ya  Mbeya na Kyela kugoma hivo baadhi ya Hiace za mjini kuamua kubeba abiria.
Hata hivyo kwa mujibu wa wachunguzi wa mambo walieleza kuwa, inaonekana ni ugeni wa barabara, speed na gari kukosa break za kuaminika.
Hata hivyo baadhi ya wadau kutoka Mbeya walieleza kuwa, Hiace imepata ajali ikiwa inatoka Mbeya kwenda Gulioni.
Bado tunaendelea kufuatilia zaidi na pindi taarifa za kina zitakazopatikana tutawaletea  hapa.
11140069_829771570393049_4114337709119012169_n
Daraja la Kiwila palipotokea ajali hiyo ya Hiace iliyoua watu zaidi ya 20.
11109302_829771647059708_1536498135139191101_n
Hiace iliyopindukia mtoni na kuua watu zaidi ya 20 huku maiti zikiendelea kuoplewa.
11170342_829771560393050_5585074619905855395_n
Wakazi wa eneo wakiendelea kumiminika kushuhudia tukio hilo.

Post a Comment

Previous Post Next Post