Baadhi
ya miili ya walipoteza maisha kwenye ajali ya gari aina ya Hiace
iliyopinduka Mtoni, ikiwa imefunikwa baada ya kuopolewa na wasamaria
wema huko, eneo la Uwanja wa Ndege, Kiwira Kyela.
Na Andrew Chale wa Modewji blog
“Tuamke
na Mungu, tutembee na Mungu. Hivi ndivyo tunavyoweza kusema kwa sasa
kufuatia hali ya ajali za mara kwa mara zinazotokea ndani ya nchi yetu”.
Asubuhi
ya leo huko Tukuyu Mkoani Mbeya imeripotiwa ajali mbaya ya Hiace
iliyoua takribani watu zaidi ya 20, eneo la Uwanja wa ndege Kiwila Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya.
Imeelezwa
kuwa, miili 22 imefanikiwa kutolewa baada ya Hiace hiyo iliyotumbukia
mtoni na bado miili miwili imenaswa, huku ikielezwa kuwa watu wawili tu
ndio wamepona akiwemo kondakta.
Ilielezwa kuwa, Ajali imetokea wakati Coaster zinazofanya safari zake kati ya Mbeya na Kyela kugoma hivo baadhi ya Hiace za mjini kuamua kubeba abiria.
Hata
hivyo kwa mujibu wa wachunguzi wa mambo walieleza kuwa, inaonekana ni
ugeni wa barabara, speed na gari kukosa break za kuaminika.
Hata hivyo baadhi ya wadau kutoka Mbeya walieleza kuwa, Hiace imepata ajali ikiwa inatoka Mbeya kwenda Gulioni.
Bado tunaendelea kufuatilia zaidi na pindi taarifa za kina zitakazopatikana tutawaletea hapa.
Vyanzo/Credit: http://habari24.blogspot.com na http://mbeyayetu.blogspot.com
Daraja la Kiwila palipotokea ajali hiyo ya Hiace iliyoua watu zaidi ya 20.
Hiace iliyopindukia mtoni na kuua watu zaidi ya 20 huku maiti zikiendelea kuoplewa.
Wakazi wa eneo wakiendelea kumiminika kushuhudia tukio hilo.
إرسال تعليق