Taarifa zilizotufikia chumba cha habari cha modewjiblog zimeeleza
kuwa Askofu Josephat Gwajima aliyejisalimisha Polisi Central na
hatimaye kupelekwa Mahakama ya Kisutu wameachiwa huru kwa dhamana yeye
pamoja na wachungaji wake watatu, jijini Dar es Salaam jioni ya leo.
Askofu Gwajima aliwataja Maaskofu hao kuwa ni Askofu Geofrey Andrew, Mchungaji George Mzava na Askofu Yeconia Bihagaze.
Hiyo
ni kufuatia kushitakiwa kwa mashitaka mawili yanayowakabili likiwemo
kumkashifu Askofu Pengo (Mshitaki ni Jamhuri, Mlalamikaji ni Abubakary
wa Kiluvya).
Kwa
upande wa tuhuma ya pili ni tuhuma za kumtorosha mtuhumiwa ambao ni hao
maaskofu watatu waliotajwa hapo juu (Mshitaki ni Jamhuri).
Hiyo
ni kufuatia Jeshi la Polisi lililofika nyumbani kwake alfajiri ya leo
kwa lengo la kumtaka kwenda kuhijiwa makao makuu ambapo hata hivyo
aliligomea kuondoka nao hadi hapo alipokuja wakili wake Peter Kibatara
na kukubali wito huo waliojipeleka wao wenyewe bila kushurutishwa majira
ya saa nane mchana leo.
Endelea kuperuzi modewjiblog kwa habari moto moto.
إرسال تعليق