Staa mwenye ‘figa’ matata, Tamrina Posh ‘Amanda’ hivi karibuni
aligeuka mbogo kwa shabiki wake aliyefahamika kwa jina la Joel baada ya
kuambiwa eti ni mmoja wa wasanii wanaotumia vidonge vya ARV vya kuongeza
siku za kuishi kwa waathirika wa Ukimwi.
Staa mwenye ‘figa’ matata, Tamrina Posh ‘Amanda’.
Ishu ilianzia kwenye mtandao wa Facebook ambapo Joel aliona picha ya
Amanda akipima ugonjwa ambao haukujulikana ndipo kijana huyo
alipokomenti kwamba eti msanii huyo ana ngoma.Akizungumza na Ijumaa,
Amanda alisema amechoshwa na watu wanaomkashifu mtandaoni wakidhani kila
msanii ni mhuni.
“Nimeona nimtolee uvivu kwani asifikirie Bongo Muvi wote tunatumia
ARV, mimi nimepima mara ya mwisho juzi na najiamini najua
ninachokifanya, alinikera sana yule kijana ndiyo maana nikampa makavu,”
alisema Amanda.
إرسال تعليق