Mambo ya fweza! Sexy lady kunako sinema za Kibongo, Jennifer Kyaka
‘Odama’ amefanya kufuru ya aina yake baada ya kumwandalia mwanaye,
Janson bonge la sherehe ya kuzaliwa (bethidei), aliyekuwa akitimiza
mwaka mmoja iliyokuwa kama harusi.
Pati
hiyo iliyohudhuriwa na mastaa kibwena Bongo ilichukua nafasi kwenye
Ukumbi wa Msasani Beach, Kinondoni jijini Dar, wikiendi iliyopita ambapo
shughuli nzima ilikuwa imeandaliwa kama harusi ambapo kwa mujibu wa
waandaaji iliteketeza mamilioni ya shilingi yanayodaiwa kumwagwa na baba
mtoto lakini mwenyewe akaingia mitini.
Kilichoweka rekodi kwenye sherehe hiyo ni pamoja na vinywaji na misosi ambayo waalikwa walikula na kunywa hadi wakasaza huku mama mlezi wa wasanii, Mama Loraa akivua saa yake ya mkononi ya dhahabu na kumpa mtoto huyo ambaye alikuwa akilia.
Baadhi ya mastaa waliotinga ni pamoja na Kajala Masanja, Halima Yahya ‘Davina’, Salome Urassa ‘Thea’, Sabrina Rupia ‘Cathy’, Mama Loraa, Zubery Mohamed ‘Niva’, Jimmy Mafufu, Herieth Chumila na wengine wengi ambao walifanya sherehe kufana vilivyo ambapo walikula na kunywa hadi baadhi yao wakawa ‘bwi’.

إرسال تعليق