Mtoto wa Kajala Masanja ‘K’, Paula Paul. |
Kazi kwelikweli! Mkali wa sinema za
Kibongo, Kajala Masanja ‘K’ amefunguka kuwa kwa umri aliofikia mwanaye,
Paula Paul wa miaka 14 ana kibarua kigumu cha kuhakikisha anakuwa salama
hasa kwenye suala la wanaume.
Akichezecha taya na Ijumaa Wikienda wikiendi iliyopita, Kajala
alisema kuwa kwa umri huo, Paula ambaye alizaa na Prodyuza wa Bongo
Records, Paul Matthysse ‘P Funky’ anahitaji uangalizi wa nguvu na
kumsimamia kwa kila jamabo ili kuwakwepa ‘mijitu mikware’ ambao wanaweza
kumrubuni.
“Dunia ya sasa watu siyo wema kihivyo lakini naamini sitashindwa na Mungu anisimamie,” alisema Kajala.
إرسال تعليق