Staa wa filamu za Kibongo, Esha Buheti amesema anajipanga kumtafuta
msanii mwenzake Issa Musa ‘Cloud’ ili amuombe msamaha akiamini bila
kufanya hivyo mambo hayawezi kumnyookea.Esha alisema yeye na Cloud ni
kama mtu na kaka yake lakini kwa hali ilivyo inaonekana kama msanii
mwenzake huyo ana kinyongo naye hivyo atakwenda kumuomba radhi ili
tofauti zao ziondoke.
Staa wa filamu za Kibongo, Esha Buheti.
“Yaani nimekaa na kuona ipo haja ya mimi kumtafuta na kumuangukia
Cloud ili kama kuna kitu nilimkwaza anisamehe kwani naona kama mambo
hayaniendei vizuri,” alisema Esha huku akidai anajua kinachomfanya Cloud
‘ammaindi’ ni kitendo cha yeye kutangaza kujitoa Bongo Muvi.
إرسال تعليق