Chama
cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Jamii nchini ‘Tanzania Bloggers
Network’ – TBN kinapenda kuwajulisha wanaotaka kujiunga na chama hicho
kuwa fomu za kujiunga zinatolewa. Wahusika ni wamiliki na waendeshaji
wote wa mitandao ya kijamii (blogs na forums) Tanzania na Watanzania
wanaofanya kazi kama hiyo nje ya nchi.
Sifa
kuu kwa mwanachama ni kuwa na blog ambayo ina umri wa miezi sita tangu
ianze kuendeshwa mfululizo. Kwa wa kazi wa Dar es Salaam wenye sifa
ambao wanataka kujiunga fomu hizo zinapatikana kwenye Ofisi za Muda za
Tanzania Bloggers Network (TBN) kwenye Jengo la Dar Free Market lililopo
mkabala na Barabara ya Ally Hassan Mwinyi.
Mwanachama
muitaji wa kujiunga kabla ya fomu atatakiwa kutoa shs 25,000/- ikiwa ni
Kiingilio cha mwanachama, shs 15,000/- yakiwa ni malipo ya ada ya miezi
mitatu kwa mwanachama na shs 10,000/- ikiwa ni malipo ya kadi ya TBN
kwa mwanachama (utambulisho). Jumla kuu kila mwanachama anatakiwa kulipa
shs 50,000/- na kupewa risiti halali ya malipo ya TBN. Fomu zitatolewa
siku za kazi kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni. Zoezi la
utoaji fomu litasimamiwa na Mweka Hazina wa TBN, Shamim Mwasha
(0767418941). Fomu pia zinapatikana Ofisi za Michuzi Media, mjini Jengo
refu karibu na Hospitali ya Ocean Road ghorofa ya pili.
Kwa
wanachama wa mikoani utaratibu unafanywa namna ya kusambaza fomu hizo
mara moja na wanachama watalipa moja kwa moja benki ya NMB kwenye
akaunti ya TBN. Utaratibu unafanywa kupata viongozi wa kanda wa muda
watakaoratibu usajili kwa kushirikiana na viongozi wa muda wa TBN taifa.
Viongozi wa muda wa mikoa na kanda watapewa maelekezo namna ya
kusimamia na kuratibu zoezi la kujiunga uwanachama wa TBN.
Mikoani
TBN itagawanyika kwa kanda, yaani Kanda ya Pwani (ikijumuisha mikoa ya
Tanga na Pwani yenyewe), Kanda ya Zanzibar (ikijumuisha Unguja na
Pemba), Kanda ya Dar es salaam, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini
(inayojumuisha mikoa ya Iringa, Mbeya, Rukwa, Simiyu), Kanda ya Kusini
(jumuisha mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma), Kanda ya Kati (mikoa ya
Dodoma, Tabora, Morogoro na Singida), Kanda ya Magharibi (inayojumuisha
mikoa ya Kigoma na Rukwa), Kanda ya Ziwa (yenye mikoa ya Kagera, Geita,
Mara na Mwanza), na Kanda ya Kaskazini (inayojumisha mikoa ya
Kilimanjaro, Arusha na Manyara).
Kwa
wahitaji unaombwa kuchukua fomu yako mapema kwani usajili wa wanachama
wa TBN utafanyika kwa muda wa wiki tatu kisha zoezi hili litafungwa ili
kutoa fursa kwa viongozi na kamati husika kutathmini wanachama
waliopatikana na litafunguliwa tena baada ya miezi sita.
NB;-
Kwa watakaohitaji katiba ya TBN watapewa pia ofisini coppy, lakini
coppy hiyo wataigharamia wenyewe. Utaratibu unafanywa wa kuichapa kwenye
soft coppy na zitatumwa mikoani kwa gharama za TBN.
Imetolewa na:
Joachim Mushi, 0756469470
Mwenyekiti wa Muda wa Tanzania Bloggers Network (TBN)
إرسال تعليق