Ikiwa kwenye misele ya mlala nje, ile Timu ya Oparesheni Fichua Maovu
(OFM) ya Global Publishers, imenasa tukio la aina yake ambapo mwanaume
aliyejitambulisha kuwa ni mume wa mtu amekutwa na mwanamke changudoa
akivaa suruali baada ya kuvunja amri ya sita ya Mungu kwenye eneo la
biashara ya mamantilie!
Wakihamaki baada ya kukurupushwa.
Tukio hilo la aina yake lilinaswa kwenye uchochoro mmoja, maeneo ya
Mwenge, Dar, majira ya saa 9:00 usiku ambapo wahusika hao ambao
hawakutaka kutaja majina walikutwa wakiwa wanavunja amri ya sita kabla
ya kushtuliwa na mwanga wa kamera za makachero wa OFM.
Wakiwa wanakatiza kwenye uchochoro huo, OFM walisikia miguno ya
kimahaba ambapo ilibidi kutulia kidogo kujua kunani kinachoendelea
mahali hapo.Waliposogelea waliwashuhudia wawili hao wakiwa wamevua nguo
ambapo mwanamke alikuwa ametandika khanga chini bila kujali mtu anaweza
kukatiza na kushuhudia sinema yao ya ngono.
Dada huyo akivaa baada ya fumanizi hilo.
Mara baada ya kuwafotoa picha kadhaa, wawili hao walishtuka huku
mwanamke akivaa nguo harakaharaka kabla ya mwenzake naye kuvaa kisha
wakataka kuanzisha timbwili kwa OFM.Wakati wawili hao wakizozana na OFM
kwa kosa la kuwakatishia ‘mambo’ yao, alitokea jamaa mmoja aliyekuwa
akilinda jirani na eneo hilo hivyo kuwapa woga wawili hao.
Hata hivyo, OFM iliwatisha kuwa eneo hilo siyo gesti wala ndani hivyo
walichokuwa wakikifanya siyo sahihi ndipo wakajikuta wakiomba yaishe
bila kurushwa gazetini.Kwa upande wake, mwanaume aliomba asamehewe
akidai kuwa ni mume wa mtu na kama tukio hilo litaenda hewani itakuwa
fedheha kwa familia yake.
“Huyu
dada yeye hana shida sana kwani siyo mke wa mtu. Tatizo lipo upande
wangu maana mkinitoa itakuwa fedheha kwa mke na watoto wangu,”
alijitetea jamaa huyo bila kujua OFM walishakula kiapo cha kutokomeza
uovu kwenye jamii.Baada ya aibu hiyo, wawili hao waliondoka mahali hapo
na kutimkia kusikojulikana.
إرسال تعليق