HOFU YATANDA, NIYONZIMA ATEMWA YANGA

Timu ya klabu ya Yanga imeondoka nchini usiku wa kuamkia leo kuelekea nchini Tunisia kucheza pambano la marudiano dhidi ya Etoile huku ikimwacha kiungo wake tegemezi Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima ambaye ni majeruhi.
Niyonzima hawezi kabisa kwenda kucheza kwa sababu bado hajapona kabisa.
Kikosi cha Yanga kilichoenda Tunisia ni hiki,
makipa
Ally Mustafa ‘Barthez’ na Deo Munishi ‘Dida’,
Mabeki
Pato Ngonyani, Oscar Joshua, Edward Charles, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, ’Juma Abdul, Rajab Zahir, Mbuyu Twite na Kevin Yondan.
Viungo
Nizar Khalfan, Andrey Coutinho, Salum Telela na Said Juma ‘Makapu’, wakati
washambuliaji
Hussein Javu, Amissi Tambwe, Kpah Sherman, Mrisho Ngasa, Jerry Tegete na Simon Msuva. 
Yanga SC inahitaji ushindi wa ugenini au sare kuanzia mabao 2-2 kufuatia kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Etoile katika mchezo wa kwanza Dar es Salaam wiki iliyopita.

Post a Comment

Previous Post Next Post